Hii ndio VPN na faida zake , je ina msaada wowote kwa Taifa ?

Hii ndio VPN na faida zake , je ina msaada wowote kwa Taifa ?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
VPN au VIRTUAL PRIVATE NETWORK ni teknolojia ambayo inakupa ulinzi na usalama wakati unatumia Internet hususani Public networks au mitandao ya Umma .

Kwa kifupi inazuia kuonekana utambulisho wa kifaa chako ambayo network husika imekipa au kitaalamu ni IP ADDRESS . Hivyo ni ngumu taarifa zako kujulikana au kuchuliwa au kifaa chako kama ni simu kuwa controlled/ kuendeshwa na mtu mwingine.

Matumizi ya VPN ni kama yafuatayo:-

1.Inakuwezesha kuperuzi tovuti zenye END TO END ENCRYPTION (E2EE) hata kwa kutumia public Wi-Fi , hii inamaana aina ya kutumia taarifa au ujumbe ambayo ina USIRI mkubwa kutoruhusu mtu mengine kupata hizo taarifa.

Mfano mzuri ni JAMIIFORUMS ,ukichukua Simu yako ukaunga Wi-Fi ya kazini au hotelini utaona inasumbua kufungua sababu hiyo network haiko secure na JF haiwezi kubali ingia huko ukiongeza ulinzi kwa VPN itafunguka sababu inatoa utambulisho mpya .

2.Inaficha utambulisho wako
Hapa ni sababu VPN inabadilisha utambulisho au IP address.

3.Inalinda haki yako ya kupata Usiri au privacy

4.Ukiwa na VPN itakupa Uhuru wa kutembelea Tovuti za Nchi mbali mbali hata kama kwa Nchi uliyopo zimefungiwa .

5.Itakusaidia kuondokana na Ubaguzi wa ki gharama unaponunua vitu mitandaoni /Online shopping

6.Na faida nyingine kama kuepuka kupitiliza matumizi ya bando , kudownload haraka ..nk .

Hivyo haya ndio baadhi ya Matumizi ya VPN ingawa ikitumika vibaya ni Hatari pia .​

Je ina msaada wowote kwa Taifa?
 
Back
Top Bottom