Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Shabaha kubwa na ya Makusudi ya ACT-WAZALENDO kumuombea Mhe Freeman Mbowe msamaha kwa Rais amsamehe kuhusu kesi yake ya tuhuma za ugaidi inaonekana chama hiki kwa kujua au kutokujua kinataka kutumika kuisafisha serikali ya awamu ya 6 baada ya kuona kua hii kesi inalitia taifa aibu.
Sasa ACT-WAZALENDO wanatumika kuisafisha serikali ili Mbowe aombe msamaha kwa Rais ionekane kuwa alikosa na hivyo ionekane ni kweli alishiriki kula njama za kufanya Ugaidi. Wanajua kabisa kua mbele ya maamuzi ya kisheria hakuna kesi hapo, ushahidi wote mpaka sasa ni shahidi wa 12 hakuna popote panathibisha ugaidi wa Mbowe. Yaani wanataka Mbowe akirinkosa ambalo hakukifanya ili wamgeuke kubwa alifanya makosa ya ugaidi waanze kukiandama chama chake kwa kukipaka matope.CHADEMA wasikubali mtego huu ambao ACT-WAZALENDO ni chanzo tu.
Lengo la ACT ni Mhe Mbowe akubali kuomba msamaha ili aonekane kweli alikuwa Gaidi, hawa hawa ACT-WAZALENDO na CCM watakigeuka CHADEMA na kukiita Chama cha magaidi, watakipaka matope na mwisho wa siku ACT kionekane chama safi na kiweze kuwa chama kikuu cha upinzani.Hii ndiyo Shabaha kuu ya ACT-WAZALENDO.
Naamini CHADEMA ni taasisi imara na ni chama kikubwa ambacho kinaifanya mambo yake kwa weledi na unafiki huu wa ACT wanaielewa vyema.
Alianza Zitto wazi wazi akamuombea msamaha Mhe Mbowe mbele za Rais kitu ambacho CHADEMA wakistuka na kumwakia juu, juzi kafiata mzee Duni bila haya anadai angewa nafasi ya kumuombea Mhe Mbowe msamaha angefanya hivyo kuliko kuendelea kukaa jela. Huu mpango si wa bahati mbaya, CHADEMA wameshaustukia. Wanachofanya ACT-WAZALENDO ni unafki ambao kesho wataujutia mbele za wananchi kwani wao ni chama kichanga sana.
Zitto Kabwe ameamua kuendesha taasisi yake kwa kujipendekeza,kutumika na kujikweza akidhani kuwa wanaweza kufika mbali. Kuwa chama kwa misingi ya uongo na unafki hakuwezi kukufikisha chama chao mbali. Wao badala hata ya kuwaongezea CHADEMA mawakili ili iwe kama kuwatia moyo leo wao wanamuombea Mtuhumiwa Msamaha wa kesi ya Kubumba ili tu apewe jina jipya la Gaidi kisha wao wanufaike.