Naomba tuongee ukweli hapa sasa hapa JF. Tatizo la matatizo ya hii nchi ni mfumo. Kinachotokea ni kwamba viongozi wanataka kuishi kwa mfumo wa kurithi kutoka kwenye historia ya enzi ya CCM chama kimoja. Viongozi wengi hasa walio mawaziri wanatoka kwenye historia ya labda baba likuaga waziri, au alishakuaga mbunge miaka kadhaa iliyopita, au alishashika nyadhifa serikalini chini ya uongozi wa CCM. Sasa tukimchukulia mfano huyu Haji Mponda, kwangu mimi ni mtu ninaye mfahamu na ni mtendaji mzuri sana sana.
Yote uliyoyasema ni sahihi, kama kuna CV iliyokaa vizuri basi ni ya Dr Hussein Haji Mponda. Ameandaliwa kiuongozi kwa Stashahada ya juu kutoka hapo Mzumbe ambacho ndicho kinachotambulika kitaifa na nje ya nchi ktk fani ya uongozi. Kwenye fani ya afya ya jamiii ana shahada ya Uzalmili na Shahada ya Uzamivu kutoka Hapo London School of Tropical Hygeine, moja kati ya vyuo bora kabisa ktk fani ya public health. Sasa wnao doubt CV hii watuambie walitaka ionyeshe amesoma wapi? Kwa uzoefu amekuwa lead reseacher kwenye eneo la malaria kama mfanyakazi wa Ifakara Healtj Institute. Kwa taarifa ya wasiojua Ifakara Health Institute ilnatambulika kimataifa kama Taasisi ya utafiti wa malaria ikishirikiana na Swiss Tropical Institute & Research Centre.
Kiutendaji ktk wizara yeye si mtendaji bali ni msimamizi wa sera. Inawezekana tatizo ni la mfumo na halitokani na Dr Haji Mponda as an individual. Tunapo discuss kwa kwa kuponda kila tuna poteza malengo.