Kwa ambao hamjawahi fika Dubai mnatakiwa kujua ule mji umegawanyika sehemu mbili. Kuna Dubai hii mpya inayoendelea kujengwa ambako ndo kuna lile jengo refu na majengo mengine mazuri ya kisasa. Zile hotel zenye Dolphins ziko upande huo. Dubai Mall pia iko huko. Picha za mleta uzi hiyo ni Dubai mpya. Matajiri kama Shilole na Kajala mdo hufikia huko.
Pia kuna Dubai ya kizamani huko Deira na Sharjah. Pale Deira ndo sisi choka mbaya huwa tunafikia. Hoteli hata kwa Tsh 70k unapata. Na kuna apartments zilizokodishwa na wabongo ambazo nao wanatulaza sisi kama vile wanafunzi kwenye madeka. Ni bei nafuu sana. Wanachaji kama Dirham 150 kwa wiki. Kimsingi huu upande wa swekeni maisha ni marahisi. Ili twende sawa na watoto wa kishua huwa tunaenda kule Dubai mpya na kupiga picha za kutosha kwa ajili. Pamoja na Deira kuwa sweken bado ni pa moto mno... pasafi hatari hakuna vumbi kabisa. Soko la vito vya dhahabu ndo liko huko Deira (Gold souk). Hata maduka ya simu mengi ya bei rahisi unayakuta Deira. Kimsingi hili ni eneo la wafanyabiashara waliofuata mizigo. Ukitaka bata panda taxi nenda mitaa ya Burj Khalifa.
Sehemu ambayo utaona uchafu na kujihisi upo bongo ni Sharjah maeneo wanapouza computer used. Mnaotaka kwenda Dubai msiogopeshwe. Ukiwa na milioni zako 3 unaenda na kurudi kwa raha zako. Milioni 3 inakava nauli, malazi na msosi.