Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Wakati dunia nzima ikishuhudia uhuni wa hali ya juu, unaofanywa na serikali ya CCM katika kuekekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu, vyama vya upinzani nchini, wananchi walio wengi pamoja na viongozi wa dini, wameendelea kutoa mwito kwa Serikali, kuuahirisha uchaguzi huo, ili kutoa fursa ya kukaa pamoja, kutafuta maridhiano kwa uchaguzi huo ambao umevuruguka kwa kiasi kikubwa sana.
Vyama vya upinzani vilivyojitoa kwenye kinyanganyiro hicho, wanadai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana, wa kanuni zinazoendesha uchaguzi ulio huru, kuanzia wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura, zoezi zima la uchukuwaji wa fomu za kugombea, hadi wakati wa kuzirejesha fomu hizo, ambapo wagombea zaidi ya asilimia 95, kutoka vyama vya upinzani, waliambiwa na hawa wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada kindakindaki wa CCM, kuwa hawana sifa za kugombea.
Wakati huo huo hao wasimamizi wa uchaguzi, wakionyesha upendeleo wa wazi kabisa kwa wagombea wa chama chao chao cha CCM, ambapo wagombea wake wote, kwa asilimia 100, wakapitishwa kuwa wagombea halali wa chama chao.
Hivi katika mazingira hayo, ubabe huu unaoonyeshwa na utawala huu wa CCM wa awamu ya tano, wa kutotaka kuwasikiliza wapinzani.hoja zao, hakika unaweza leta machafuko makubwa sana ndani ya nchi hii.
Ifahamike pia kuwa, uchaguzi ulio huru na haki, kwa kutumia sanduku la kura ndiyo njia pekee na iliyo salama zaidi ya kudumisha hali ya amani na utulivu katika nchi yetu.
Inaonekana wazi kuwa watawala wetu wamelewa waadaraka na wameamua kuweka pamba masikioni na kutotaka kusikiliza maridhiano ya aina yoyote na vyama vya upinzani yanafikiwa na badala yake wamekuwa wakitoa vitisho vya hali ya juu, kuwa yeyote atakayeleta fujo wakati wa uchaguzi, Jeshi la Polisi nchini "limeagizwa" na watawala wetu, wawashughulikie kikamilifu.
Hivi ni kwanini watawala wetu wameamua kulewa madaraka kiasi hicho?
Katika uchaguzi ambao dunia nzima inauona kuwa wapinzani wa nchi hii wamefanyiwa hila nyingi, ni kwanini hawataki kuuahirisha na kukaa meza moja na wapinzani na kuwasikiliza wapinzani hao ili kufikia maridhiano?
Hivi huu utawala utaendelea kulitumia hilo Jeshi "lao" la Polisi kukandamiza haki za msingi za raia hadi lini?
Ndiyo maana nikasema vyama vya siasa vya upinzani ni vyema vikaitumia hii fursa bila ya kukata tamaa kudai hiyo Tume ya uchaguzi iliyo huru.
Siyo vyema hata kidogo kukata tamaa na kutishwa na hilo Jeshi "lao" la Polisi nchini, kwani mamilioni ya Umma wa watanzania yapo nyuma yenu, katika kudai Tume hiyo iliyo huru, hadi ipatikane.