Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Siku Rais Samia alipomteua Mchengerwa kuwa Waziri wa TAMISEMI, alimsifia kuwa Mchengerwa ana kifua kipana!! Kila mmoja alitoka na tafsiri yake juu ya kauli hiyo ya Rais Samia. Lakini wengi tulidhania kuwa kifua kipana cha Mchengerwa, japo hatujawahi kukiona, Rais alikuwa akimaanisha uwezo wa Mchengerwa katika kupigania kufanikisha mambo mazuri. Kumbe tulikosea sana.
Yanayoendelea sasa kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, uchaguzi unaosimamiwa na waziri Mchengerwa, sasa tunapata maana halisi aliyoimaanisha Rais Samia. Kifua kipana cha Mchengerwa, kwa kuzingatia maovu yanayoendelea:
1. Kuandikisha watoto wa shule ambao hawajafikisha umri wa kupiga kura.
2. Kutoa takwimu za uwongo za watu waliojiandikisha kupiga kura, kama zile za kuonesha wananchi wote wa Dar na Mwanza (rejea takwimu za sensa), mpaka waliokuwa watoto wa chini ya miaka mitano wakati wa sensa, sasa wamejiandikisha kupiga kura.
3) Kuengua wagombea karibu wote wa kutoka vyama vya upinzani.
4) Kuwaambia walioenguliwa wakate rufaa, huku kukiwa na maelekezo kwa wasimamizi wa uchaguzi wafunge ofisi, ili wanaokata rufaa, rufaa zao zikose mtu wa kuzipokea,
bila shaka kifua kipana cha Mchengerwa ni katika kusimamia uovu bila aibu wala woga.
Uharamia unaofanyika sasa dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani, ni ule ule wa mwaka 2019. Mwaka ule lawama zote zilikuwa kwa hayati Magufuli, kuwa ndiye aliyelekeza wapinzani wote waenguliwe. Je, huu uharamia wa sasa, ina maana ni maelekezo ya Rais Samia, kupitia huyu Waziri mwanafamilia wake?
Utawala wa Rais Samia, kila mara ulijipambanua ni utawala bora zaidi katika demokrasia na haki kuliko hayati Magufuli, je, huo uzuri ni upi? Wagombea wa upinzani wameenguliwa kama wakati wa Rais Magufuli, wakosoaji wa Rais Samia wametekwa na kupotezwa kama wakati wa hayati Magufuli. Wakati wa hayati Magufuli, mkosoaji mkuu Tindu Lisu alishambuliwa na kunusurika kifo, lakini wakati wa Samia Ali Kibao alitekwa na kuuawa.
Je, huu utawala una jema lipi kuuzidi utawala wa Hayati Magufuli?
Pamoja na tunayomlaumu hayati Magufuli, lakini angalao kuna vitu vizuri alivyovifanya, vipo na vinaonekana.