Folk Part II
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 419
- 490
Atakuwa alikutana na kishombo cha samaki kama alikukimbia niamini mimi wala si kingine au ulimpimia bando sana ukampa kiduchuIlikuwa siku mmoja nilikuwa kwenye mapenzi na kijana mmoja wa mwanza tulikutana ofisi fulani baada ya mazoea ya pale aliomba namba nikampa tukawa tunawasiliana kawawaid kila siku mpaka nikajikuta nimeingia kwenye mapenzi nikajikuta nampenda sana mimi na wivu jamani ukiwa na mimi unatakiwa uwe mvumilivu kidogo.
Tulipanga siku ya mimi kwenda Mwanza, siku ilipofika nilijipanga vizuri nikiwa na bashasha nyingi sana ya kukutana nae na kutokana na utani mwingi kipindi cha nyuma nikawa naona safari ndefu sana.
Baada ya kufika siku ya kwanza alinipokea akanipeleka hotel nzuri tu, nililala nae usiku mzima kesho yake morng aliniaga anaenda kazini alinipa pesa ya dharura laki moja kumbee chumba hajalipa nimekaa pale siku tatu mtu hajatokea nikipiga simu apokei kisa sikijui nililipa na kurudi zangu kwetu bila kumpa taarifa.
Ndipo nilipofika akaanza jiongelesha oh mimi nilikuwa nimebanwa simu iliisha chaji samahani ulitumia kiasi gani nikupe niliona upumbavu nikakata simu, mpaka leo siwezi kumsafiria mwanaume hata awe nakaa nae mkoa mmoja ila wilaya tofauti siwezi.
Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app