Hii ndiyo sababu kwa nini wanawake wengi wanaipenda movie ya "TITANIC"

mkuu wewe ni mtu wa mkoa wa Mara?
 
Ww jamaa bhana 😂

Nadhani h titanic unayoisema hapa sip titanic h ambayo sisi wngn tunaijua
Ndio iyo iyo. Ile movie imesukwa katika namna ya kutaka kuonyesha yule mchumba wa Rose ndie villain. Lakini ukiingilia kwa fikra huru unaona villain ni Rose.

Pata picha aliyoyafanya Rose angeyafanya yule mchumba ake. Yaani Cal Hockley ndie angecheat na mwanamke mwingine mule ndani ya meli na angejaribu kutoloka nae, unafikiri angeonekana ndie steringi wa movie kama ilivyokua kwa Rose?
 
Kaitazame tena, yule hakuwa mume wa jack, ni mchumba ambae hakumpenda, akaja kumzimikia muhuni jack.. rose hawezi kuwa villain.. yule mchumba wa lazima ndio anawezekana kuonekana kama adui mkuu
Mkuu embu tuambie katika ile movie kosa la mchumba wake Rose ni lipi
 
Uzi ufungwe
 

Angalia hapo kwenye bold, ukatili wa mama yako kwa baba yako anaujua baba yako. Na baba yako angekuambia ungemchukia mama yako milele. Ila kwa vile wanaume tuna tabia ya kuweka mambo as if nothing happened, basi tunapotezea ili mradi maisha yaende.
 
Hakumcheat ila alimkataa mchana kweupeeeeee, jamaa alipambana arudi ilishindikana mwisho wa siku akakubali kishingo upande, kwa hiyo Rose alifata Moyo wake hakua na tamaa za mali kama familia yake.
 
Kuforce mapenzi, akajaribu hadi kuua etc.
Umemchumbia mwanamke. Umemchukua rasmi kutoka kwao. Mpo ndani ya meli na familia yake inajua binti yao yupo mikononi mwako, halafu katikati ya safari anatokea muhuni anataka kumtorosha. Hivi hata ungekua wewe ungewaachia tu waondoke.

Chukulia wewe ndie baba wa Rose, unajua binti yako yupo safarini na mchumba wake, halafu mume mtarajiwa wa binti yako katoka safarini anakwambia binti yako alikutana na kijana ndani ya meli nikawaachia waondoke pamoja. Ungeweza kumuelewa huyu mkwe wako?

Sijaona kosa la mchumba wa Rose. Yeye kama mume mtarajiwa alikua na dhamana ya usalama wa mchumba wake kwaiyo alifanya kile kinachostahili.
 
Kwahiyo mlitaka Rose aolewe na yule jamaa mkatili tena kwa kulazimishwa? Mna matatizo nyie viumbe
Alitakiwa kukataa kuanzia mwanzo au kama aligundua badae akiwa tayari ashakosea kufanya maamuzi basi angefuata utaratibu rasmi wa kuvunja uchumba.

Wakati wa angagement bila kushikiwa bunduki aliulizwa will you marry me? Akajibu yes akavalishwa pete, kwaiyo kuanzia hapo alitakiwa kuwa mwaminifu kwa mchumba wake. Rose alimcheat mchumba wake mule ndani ya meli, hakuna justification yoyote ya kutetea usaliti alioufanya.

Ndoa au uchumba umekushinda vunja kwa taratibu rasmi. Kumcheat mchumba/mume wako sio suluhisho bali ni kuongeza tatizo jingine
 
Hakumcheat ila alimkataa mchana kweupeeeeee, jamaa alipambana arudi ilishindikana mwisho wa siku akakubali kishingo upande, kwa hiyo Rose alifata Moyo wake hakua na tamaa za mali kama familia yake.
Rose alimcheat mchumba wake. Kuvunja uchumba kuna taratibu zake ikiwemo kurudisha engegement ring. Wakati rose anamvulia nguo jack ili amchore alikua amevaa pete ya uchumba mkononi. Baada ya pale kuna scene ambazo Rose alionekana hajavaa pete lakini hakuna scene ambayo Rose alirudisha engagement ring.

Mimi sikatai kwamba uenda Rose akua na mapenzi kwa mchumba wake. Ninachosema hapa ni ukweli kwamba Rose alifanya usaliti. Suala la kumpenda au kutompenda ingewezekana kumalizwa kuungwana. Angesubiri safari iishe wakae waongee na mchumba ake walimalizane, then aanze mapenzi yao na jack, lakini sio kumsaliti mwenzako.
 
Rose alikua malaya tu kama walivyo akina Gigy Money
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…