Hii ndiyo siri GSM kujiondoa katika udhamini ligi kuu, Simba inahusika

Hii ndiyo siri GSM kujiondoa katika udhamini ligi kuu, Simba inahusika

Inaonekana licha na malengo ya kudhamini ligi,lengo kuu ilikuwa kutangazwa na ‘Simba’ zaidi kuliko timu nyingne. Nawapongeza,ukiona lengo halijatimia huna budi kukaa pembeni.
hana pesa
 
Unadhani GSM anahasara maana Yanga pekee inatosha kumtangaza nchi nzima kama unabisha kunya kwenye Lami.
hana pesa

CA73CCAB-1D5A-416D-ACA0-16B5CA3AC793.png
 
Sasa kama mchakato ulikubaliwa na FCC, kwa nini ajitoe sasa? Aache longolongo, awape mpunga wao madogo watamtangazia brand yake humuhumu nchini
Mwambieni Mudi awe mdhamini sasa.
 
Kabla GSM kuingia makubaliano na tff hakujua kuwa utopolo wanaweza mtangaza nchi nzima
Unadhani GSM anahasara maana Yanga pekee inatosha kumtangaza nchi nzima kama unabisha kunya kwenye Lami.
 
Barbara ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba ndiye ambaye alilishikilia bango suala hilo kwa niaba ya klabu na kuiandikia barua TFF, pia klabu yake haikushiriki katika kuvaa jezi zenye nembo ya GSM.
yaani hiki kidem kitaua soka la bongo, wait and see
 
Hii ndiyo janja janja tunayosema.
Kwa hiyo thamani iliyowekwa kwa udhamini haiwezi kuleta faida isipokuwa Simba akivaa nembo ya GSM?

Kwa hiyo mlengwa wa kuubeba udhamini huo alikuwa Simba?

Kama walijua bila Simba udhamini hauna maana,kwa nini hawakuishirikisha mapema?
Kampuni ya GSM imetangaza kujiondoa katika udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hiyo siyo habari mpya kwa sasa, lakini kilichopo nyuma ya pazia na sababu kubwa ni wapinzani wao wa jadi Simba kugoma kuunga mkono juu ya udhamini huo.

Mara baada ya TFF kutangaza udhamini huo, kisha ikaelezwa kuwa klabu zote shiriki katika ligi hiyo kutakiwa kuvaa jezi zenye nembo ya GSM, Simba wao waliibuka na hoja kadhaa kisha wakagoma kutii maelekezo hayo ya TFF na Bodi ya Ligi.

Moja kati ya hoja za Simba ilikuwa ni kutoshirikishwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, GSM kuwa ni mdhamini wa Yanga wakati huohuo kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu na nyingine kadhaa.

Barbara ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba ndiye ambaye alilishikilia bango suala hilo kwa niaba ya klabu na kuiandikia barua TFF, pia klabu yake haikushiriki katika kuvaa jezi zenye nembo ya GSM.

Licha ya kuwa GSM hawajasema wazi kuhusu masharti ya mkataba ambayo wanaona yamekiukwa katika makubalano yao lakini ni wazi kuwa Simba ndiyo sababu hasa ya wao kuamua kujiondoa.

Chanzo kutoka GSM kimeeleza kuwa kitendo cha Simba kugomea kuvaa jezi zenye ‘brand’ ya GSM kisha TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kuwachukulia hatua, huku kesi ya udhamini wao ikipelekwa FCC ndiyo sababu ya kuamua kujiondoa.

Kesi hiyo ilifikishwa FCC kwa kuwa serikali iliamua kuingilia kuona kama mchakato wa fair competition ulikuwa katika njia sahihi.
 
Kumbe GSM hawajawahi kutoa hata 100 wakati club zilikuwa zinavaa nembo, huu ni udhamini hewa bora hata waondoke.
Watajua wenyewe hivyo Timu baada kusikilizia wakubwa (Simba SC) wanasema wao wanakurupuka tu.
 
GSM ni matapeli wa mpira yanga wajiandae kisaikolojia
Hawa ni matapeli toka kitambo kumbuka hawa ndo HSC..wana watu wa kupiga porojo kuwa wana hela..!

Ilitakiwa wawalipe vilabu vilivyovaa nembo kisha ndo wangejitoe.
 
Kanuni za ligi zinasema Club ni lazima ivae logo ya mdhamini mkuu kwenye bega la kushoto na sio ivae logo ya mdhamini mwenza.

Tff na GSM walishachemka, hakukuwa na kipengele cha utambuzi wa mdhamini mwenza.
 
Tuliwaambia haya yote lakini ni wachache walioelewa, tukapingwa tulitoa ufafanuzi...!

Kazi kwao kuitema Ndoano...!
 
Inaonekana licha na malengo ya kudhamini ligi,lengo kuu ilikuwa kutangazwa na ‘Simba’ zaidi kuliko timu nyingne. Nawapongeza,ukiona lengo halijatimia huna budi kukaa pembeni.
Kibaya Zaid walimtarget Simba alafu ajabu wakamtuma manara awakejeri hao hao wanaowategemea kwenye dili lao.

Manara asingeharisha Ile siku huenda Simba angekubali ,lakin zile Tambo za manara na kejer na kulifanya lile swala la udhamin Ni la yanga ndipo Simba alishtuka jumla jumla.

Mdomo ,mdomo ,mdomo wa manara ndio uliharibu hili dili tokea cku nyingi.

Manara akaona hiyo ndio njia pekee ya kumalizia hasira zake kwa Simba asijue anharibu dili mazima.

GSM wasitafute mchawi ,mchawi wao Ni manara ,Kama walimtuma au hawakumtuma aseme vile Ni wao wenyewe na akili zao.

Kwenye dili Kama lile GSM walitakiwa wacheze kimafia Sana kwa kuwa kimya na kutopiga kelele.
Pia GSM Ile cku hawakupaswa kuongozana na akina injinia na manara na kuwaweka front line ,hili Ni kosa la viwango kuwah tokea.

Kuna muda unaona watu wako smart kumbe zero kabisa ,hata Mimi huu Mchongo ningepewa nisingeweza kuucheza km walivyoucheza GSM kampuni kubwa namna Ile.
Haya ndio madhara ya kuwa na Watu wasio na upeo wa Mambo .
 
Back
Top Bottom