Kampuni ya GSM imetangaza kujiondoa katika udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hiyo siyo habari mpya kwa sasa, lakini kilichopo nyuma ya pazia na sababu kubwa ni wapinzani wao wa jadi Simba kugoma kuunga mkono juu ya udhamini huo.
Mara baada ya TFF kutangaza udhamini huo, kisha ikaelezwa kuwa klabu zote shiriki katika ligi hiyo kutakiwa kuvaa jezi zenye nembo ya GSM, Simba wao waliibuka na hoja kadhaa kisha wakagoma kutii maelekezo hayo ya TFF na Bodi ya Ligi.
Moja kati ya hoja za Simba ilikuwa ni kutoshirikishwa wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo, GSM kuwa ni mdhamini wa Yanga wakati huohuo kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu na nyingine kadhaa.
Barbara ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba ndiye ambaye alilishikilia bango suala hilo kwa niaba ya klabu na kuiandikia barua TFF, pia klabu yake haikushiriki katika kuvaa jezi zenye nembo ya GSM.
Licha ya kuwa GSM hawajasema wazi kuhusu masharti ya mkataba ambayo wanaona yamekiukwa katika makubalano yao lakini ni wazi kuwa Simba ndiyo sababu hasa ya wao kuamua kujiondoa.
Chanzo kutoka GSM kimeeleza kuwa kitendo cha Simba kugomea kuvaa jezi zenye ‘brand’ ya GSM kisha TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kuwachukulia hatua, huku kesi ya udhamini wao ikipelekwa FCC ndiyo sababu ya kuamua kujiondoa.
Kesi hiyo ilifikishwa FCC kwa kuwa serikali iliamua kuingilia kuona kama mchakato wa fair competition ulikuwa katika njia sahihi.
[
https://res]
MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni
mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.
Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi
kwa undani.
“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.
“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa
kazi kisheria,” alisema Mnguto.
Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi
baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini
kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.
“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa
kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara
ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.