Pia Mbeya ni kilimo kwa kwenda mbele karibia wilaya zote zinarutuba hali ambayo inapelekea wananchi wake kuwa na pato.Shughuli za kibiashara na kilimo zimeongezeka kwa kiasi kikubwa sana Mbeya katika miaka mitano iliyopita. Wafanyabiashara wameongezeka sana, hata lile gap lililoachwa na wafanyabiashara waliohamia hapa Dar hasa Kariakoo kukwepa kadhia ya TRA miaka iliyopita limezibwa kabisa. Mpaka wa Tunduma umerahisha sana ufanyaji biashara na Congo pia.
