HII ndo Mikoa tajiri Tanzania (Kwa mujibu wa BOT), Mbeya yaishinda Arusha...

Pia Mbeya ni kilimo kwa kwenda mbele karibia wilaya zote zinarutuba hali ambayo inapelekea wananchi wake kuwa na pato.
 

Hapo kwenye nyekundu, wakati wao wanafanya PEOPLEEEES POOOOWER, wenzao wanazalisha na kukuza uchumi. Nachangamsha baraza tu usinipige mawe
 
Inavyonishangaza mm nikuwa wakulima wako duni kimaisha wala hawapatiwi vitendea kazi kwa kilimo chao
wao wanaona tu kulipatia taifa pesa za kigeni sijui watafunguka liini macho hawa mabot kuwasaidia wakulima
kwa pembejeo za kisasa yaan kero tu hapa
 

Mazeee, mbeya iko bize sana. Tatizo Arusha ina utalii mwingi ila promo hamna, hivyo tunaishia kusema maneno ya mdomoni kwamba arusha ina utalii na inatakiwa iingize pesa, Tunduma ndugu pako bize balaaaaa. Pesa inazunguka pale balaaa.
 
Mazeee, mbeya iko bize sana. Tatizo Arusha ina utalii mwingi ila promo hamna, hivyo tunaishia kusema maneno ya mdomoni kwamba arusha ina utalii na inatakiwa iingize pesa, Tunduma ndugu pako bize balaaaaa. Pesa inazunguka pale balaaa.

Hata wale wachenji hela nao wanapiga pesa.
Nalog off
 
Mkuu huu utafiti BoT wamefanya wenyewe au wametumia REDET(Namaanisha lile shirika linalofanyaga utafiti uchaguzi ukikaribia)mbona kama data hazijatulia.
 
Hapo kwenye nyekundu, wakati wao wanafanya PEOPLEEEES POOOOWER, wenzao wanazalisha na kukuza uchumi. Nachangamsha baraza tu usinipige mawe
Na hilo ndilo lengo la utafiti huu,ili kisemwe hicho unachokisema maana uchaguzi unakaribia.
Kama BoT ni wanaume mbona wanatutengenezea mifedha haina viwango,noti ya mia tano shida,sarafu ya 50 na 100 balaa nao siku hizi wamejiunga na peoples power?
 
Jamani tusipuuze /kupinga matokeo ya utafiti kwa sababu hayajaja kama vile tulivyotaka sisi...ilipotangazwa Rostam Aziz ni tajiri kuliko Bakhresa wapo waliopinga kwa sababu waliamini Bakhresa ni tajiri zaidi ya Rostam....Big up sana Mbeya kazeni buti
 
Huwa tunawaambia Mabilionea wa Arusha ni wajanja wajanja tu mtu akiwa na gorofa 2 basi anatukuuuzwa bilionea ukienda Kariakoo hapo unakuta mkinga ana gorofa 4 na hajulikani kama Bilionea na wala watu hawamtukuzi kila mtu na 50 zake.

arusha kelele mingi nakujirusha sana wakati mbeya mkinga anapesa yake na ametulia hata huwezi kumjua.
 
Kilimo kinaibeba sana Mbeya. Big up sana. Though Arusha mjini imejengeka sana kuliko Mbeya mjini ikiwa na hoteli nyingi, majengo mengi, taasisi nyingi mfano Eac,Selian,Mandela,Aicc,Iaa,Tumaini,jkuat,tawiri,n.k,pamoja na kumbi nyingi za starehe hvo kuufanya mji kua modern zaidi ya Mbeya in my opinion.
 
nyinyi bot huu ni upuuzi tu hii inamsaidia nn mkulima wa kijiji anaetumia jembe la mkono kule kijijini acheni kupumbaza watu mnatuletea uchumi wa makalatasi

= makaratasi

Ikiwa Kiswahili ni namna hii, sijui kama umeelewa kilichoandikwa kwa lugha ya kigeni!
 
Watu mnabishana na report y BOT come up with your own report sio blah blah.
Kwa kifupi Arusha kushika nafasi ile ni ishara kuwa Tanzania tunapigwa kwenye madini na utalii
 
Na hilo ndilo lengo la utafiti huu,ili kisemwe hicho unachokisema maana uchaguzi unakaribia.
Kama BoT ni wanaume mbona wanatutengenezea mifedha haina viwango,noti ya mia tano shida,sarafu ya 50 na 100 balaa nao siku hizi wamejiunga na peoples power?

Wakilitumia hili watakuwa wamebug kinoma maana Mbeya nako ni pipoz pawa but mambo ni mswano. Ccm ni wajinga lakini si kiasi hicho mkuu!
 
lakini wadau,mimi mbeya naijua in and out,the only problem ni wanasiasa na mamlaka kuzuia ujenzi kwa kisingizio cha bonde la UFA,lakini mbeya iko juu,kumbukeni agriculture sectos is more powerful in outcome than Mining sector and Tourism sector.na hata hivyo Hotel can be there but sales can not stand all the time in base of high and low seasonability.Kumbukeni Mbozi ni very strong in income,huwezi linganisha na wilaya nyingi za arusha,so take it or live it.
 
For that matter wamachinga tulikuwa tuko sawa kugoma gesi kusafirishwa kwenda dar! Inauma sana
 
Nimetamani kuibua hii topic. Watu walikuwa wanaitetea sana Arusha kwa kuzidiwa na Mbeya, ingawa Shinyanga, Iringa na Morogoro nazo zilikuwa juu yao lakini haikuwa ikiwasumbua. Wewe F unalalamika kwanini B awe wa pili, wakati kuna C, D, E juu yako. Si ungeanza kuuliza kwanini E yupo juu yako, then wapanda hatua kwa hatua. Mabilionea wa Arusha!!! Pesa ndogo, sifa mingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…