Katika art ya history taking kwa mgonjwa, ambayo inahusisha mazungumzo, vipimo vya mkono(physical examination ) pamoja na vipimo vya maabara (lab.investigation) baada Daktari unakuja na majibu ya mwisho kutokana na vipimo vyako, sasa kwenye kuutambua ugonjwa yaani Diagnosis kuna approach 3.. ya kwanza ni Provision diagnosis hii ni ile unayodhan wewe kabla ya vipimo, ya 2 ni differential diagnosis hii ni zile zingine unazozidhan na ya 3 ni diagnosis hii ni ile ambayo vipimo vimethibitisha, na kwenye kutibu pia unaweza ukatibu symptoms yaani dalili ili kumpa relief mgonjwa mfano pain etc endapo hujapata hasa nini anachoumwa mgonjwa wako, sasa ukimwambia relative kwamba mimi nadhani huyu mgonjwa wako ana shida ya spleen ila nenda mbele kwa vipimo zaidi yeye anatoka pale moja kwa moja akijua mgonjwa wake ana shida ya spleen, sio hivyo jaman, na naamin hapakuwa na vipimo vya kutosha vyenye uwezo kugundua hasa kwa 100% ni ugonjwa gan anaosumbuliwa nao, na haya yapo tu. Mwili wa mtu ni zaidi ya msitu wa Congo sio rahis kuuelewa wote bila msaada wa vipimo. Mtuamini tupo vizuri. Mungu amponye huyo binti. "WE TREAT AND GOD HEALS"