Hii ndo Zaburi ya 35 aliyotwambia tusome Halima Mdee

Hii ndo Zaburi ya 35 aliyotwambia tusome Halima Mdee

askofu rashid

Member
Joined
Oct 26, 2020
Posts
25
Reaction score
43

ZABURI 35​

Kuomba msaada
(Zaburi ya Daudi)

1 Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.

2 Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!

3 Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4 Waone haya na kuaibika,
hao wanaoyanyemelea maisha yangu!
Warudishwe nyuma kwa aibu,
hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6 Njia yao iwe ya giza na utelezi,
wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7 Maana walinitegea mitego bila sababu;
walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8 Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,
wanaswe katika mtego wao wenyewe,
watumbukie humo na kuangamia!

9 Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;
nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10 Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:
“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!
Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,
maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.

11 Mashahidi wakorofi wanajitokeza;
wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12 Wananilipa mema yangu kwa mabaya;
nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa,
mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;
nilijitesa kwa kujinyima chakula.
Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14 kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.
Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,
kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15 Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.
Walikusanyika pamoja dhidi yangu.
Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,
wala hakuna aliyewazuia.

16 Watu ambao huwadhihaki vilema,
walinisagia meno yao kwa chuki.

17 Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?
Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;
uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18 Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;
nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19 Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,
hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20 Maneno wasemayo si ya amani,
wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21 Wananishtaki kwa sauti:
“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,
usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,
usikae mbali nami.

23 Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;
uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

24 Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,
ufanye kulingana na uadilifu wako;
usiwaache maadui zangu wanisimange.

25 Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”
Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”

26 Waache hao wanaofurahia maafa yangu,
washindwe wote na kufedheheka.
Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,
waone haya na kuaibika.

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,
wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:
“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!
Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

28 Hapo nami nitatangaza uadilifu wako;
nitasema sifa zako mchana kutwa.

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
 
Mtu yeyote anaenda shule ili aje aishi maisha mazuri, kwakuwa Elimu ndiyo urithi wa kudumu

Pia hiyohiyo Elimu Ina namna na nyanja za kutumia, iwe uanaharakati, uanasiasa, udaktari n.k.

Lengo likiwa uishi maisha mazuri, Sasa mtu anapewa uwakilishi bungeni,sehemu ambayo unapaswa uwe na ushawishi kwa wananchi au uwe na kitu kichwani.

Piga kazi Halima, ziishi ndoto ulizoziota miaka mingi, huo ndio utafutaji wa maisha.

Povu ruksa,samahani wana CDM siko chama chochote jamani

hapa nazungumzia namna ya kutumia elimu yako, uliyoipata kwa jasho
 
Hivi kuna biblia ngapi?View attachment 1639058View attachment 1639059View attachment 1639060
Screenshot_20201201-113432.jpg

View attachment 1639064View attachment 1639065
 
ZABURI 35​

Kuomba msaada
(Zaburi ya Daudi)

1 Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.

2 Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!

3 Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4 Waone haya na kuaibika,
hao wanaoyanyemelea maisha yangu!
Warudishwe nyuma kwa aibu,
hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6 Njia yao iwe ya giza na utelezi,
wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7 Maana walinitegea mitego bila sababu;
walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8 Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,
wanaswe katika mtego wao wenyewe,
watumbukie humo na kuangamia!

9 Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;
nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10 Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:
“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!
Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,
maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.

11 Mashahidi wakorofi wanajitokeza;
wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12 Wananilipa mema yangu kwa mabaya;
nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa,
mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;
nilijitesa kwa kujinyima chakula.
Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14 kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.
Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,
kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15 Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.
Walikusanyika pamoja dhidi yangu.
Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,
wala hakuna aliyewazuia.

16 Watu ambao huwadhihaki vilema,
walinisagia meno yao kwa chuki.

17 Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?
Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;
uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18 Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;
nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19 Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,
hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20 Maneno wasemayo si ya amani,
wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21 Wananishtaki kwa sauti:
“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,
usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,
usikae mbali nami.

23 Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;
uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

24 Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,
ufanye kulingana na uadilifu wako;
usiwaache maadui zangu wanisimange.

25 Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”
Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”

26 Waache hao wanaofurahia maafa yangu,
washindwe wote na kufedheheka.
Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,
waone haya na kuaibika.

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,
wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:
“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!
Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

28 Hapo nami nitatangaza uadilifu wako;
nitasema sifa zako mchana kutwa.
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Mwambie naye asome ZABURI 1: 1 - 6.

1.Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2.Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3.Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

4.Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5.Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6.Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.
 
Watu wamekariri tu Zaburi 35, wasijue kuwa katika Agano Jipya Bwana Yesu alituambia tuwapende adui zetu. Mtu akikupiga shavu la kushoto unapaswa umgeuzie na la kulia ili nalo alitandike.

KWA kifupi, katika Agano Jipya (damu ya Yesu) hatuna maadui.

KWA hakika YESU NI MWOKOZI.
 
Back
Top Bottom