Hii ni biashara ya familia au utemi?

Hii ni biashara ya familia au utemi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nineajiriwa kwenye shirika moja la serikali ambalo tunahudumia wafanya biashara kadha na kadha, nipp lwenye kitengo cha accounts kwa hio wengi wao najua hali zao kwenye faida, madeni, sales, n.k.

Katika moja wapo ya wafanya biashara kuna mfanya biashara kiukweli yupo fresh, si haba, nje ya kumjua ofisini pia anakaa mtaa ambao haupo mbali sana napoishi kwa hio namjua kwa kiasi flani

Faida yake kwa mwezi ni kama milioni 20 baada ya kutoa gharama, nina uhakika na hili maana mimi nipo department ya accounts. Sasa hii ni biashara ya familia, kuna wadogo zake kadhaa na ndugu zake kama wanne hivi na wafanyakazi wengine wachache.

Mishahara inacheza kwenye laki 1 hadi tatu, chakula huwa kinaletwa hivyo hawagharamiki, kiukweli nilishangaa sana hapa. Kinachonishangaza zaidi mtu yupo proud sana kwamba family business anasaidiana na wanafamilia ila ukicheki hapo unaona kabisa kwa hio mishahara ni ngumu kwa wengine kupiga hatua

Yaani kusema hata kuona kuna wanafamilia au ndugu zake kuwaona na gari au piki piki hakuna, ila yeye gari anazo za kubadilisha.

Hivi hii ni family business au?
 
Hao family members ni shareholders ama waajiriwa?

Yaani unafanya kazi kwa blazeri alafu unasema ni family business?
 
Ukiwa Finance unapswa uwe na kaba... la sivyo utaanza udokozi...
 
Back
Top Bottom