Hii ni CCM toleo la 4 na la mwisho; hakuna CCM nyingine baada ya hii!

Sasa Chadema ndo wamekuwa wapiga shangwe kwa mama huku wakisema CCM inakufa lakini nikiri wazi kuwa kweli CCM wasipojiangalia wataanza kuzomewa tena mitaani wakivaa nguo zao.
 
Mama hagombei kwa legacy yake...kitawekwa chuma ambacho bila shaka bavicha hamtakipenda, mama akigombea hata mie simpigii kura, wala sitapiga kura ya urais akigombea..
Atawekwa hussein mwinyi au chuma majaliwa
 
Sasa Chadema ndo wamekuwa wapiga shangwe kwa mama huku wakisema CCM inakufa lakini nikiri wazi kuwa kweli CCM wasipojiangalia wataanza kuzomewa tena mitaani wakivaa nguo zao.
Inachekesha sana...
 
Hahahaaa,kwa wema gani mlio nao
 
Nilichogundua kuna watu wanaumia, ila wanajifanya wako ngangari na kuwatupia mizigo ya maumivu wengine. Hawapendi kumuona mtu katoka kwao kisha anahamia upande mwingine na anakula shavu. Wanaanza kuwacheka waliokosa ili ionekane wao ni fungu la kukosa ili wanune wote.
Ukweli ni kua ndani ya chama tawala kuna fursa, watu wanatafutia majina upinzani kisha wanaenda kula vizuri kwenye chama tawala. Hiki kitendo kinawaumiza sana upinzani, wanakosa dira, mara wacheke mara wanune. Siasa ni ngumu kuliko physics.
 
Kama vyombo vya Ulinzi na Usalama vinamkubali atapeta tu! Rais wa Tanzania kwa sasa hachaguliwi na wapiga kura kwenye Sanduku la Kura.Hapa ndipo penye shida kwa nchi yetu.
 
Hii comment yako ihifadhiwe.

Ukweli unaokuja ndio huu
 
Uko uvccm nini mbona povu jingi , sio kwli kua mnalia , wengi wenu mlikua mnasubiria teuzi , mnaumia kuona wahamiaji na waandishi wa habari ndio wanaonekana
Sijawahi and sitegemei. Ila mnsikitisha mnavotumia nguvu kuwananga UVCCM wakati karibia 95/% ya wateule ni vijana ambao obviously ni UVCCM
 
Mshana Jr
 
Uteuzi wa Nassari,Lijuakali nk umewauma sana bavicha kwani unabii wenu hasi umeanguka.Kufa hamtakufa ila cha moto mtakiona
 
Ila mkuu Mimi Kuna Jambo sielewi kwamba nafasi za teuzi lazima ziwe based kwenye Chama ,au kuangalia uwezo wa mtu bila kujali anatoka wapi,

Binafsi siungi mkono teuzi za watu wasikua na uwezo Kama ambavyo naona teuzi za WAKUU wa WILAYA baadhi ila naunga mkono kwamba Chama chochote kiwapo madarakani basi teuzi sio lazima ziwe based kwa Chama atokacho bali uwezo
 
Vp wewe hujapata teuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…