Hii ni CCM toleo la 4 na la mwisho; hakuna CCM nyingine baada ya hii!

Bila kuwasahau mataga wakuu , Pascal Mayala , johnthebaptist, magonjwa mtambuka , Crimea , Stroke , Mama D , mpaka huruma .
namimi umenisahau.

ajabu walioachwa wengine maumivu mnapata chadema[emoji23][emoji23],hii dunia bana daah.
 
Mshana katika ubora wake! Brilliant Analysis. JPM "aliiua" CCM kwa kupunguza madaraka ya Halmashauri Kuu ya CCM, Secretariat ya CCM pia kuwaondoa viongozi asilia wa chama, kuwatenga viongozi wa zamani. Akaizika kabisa alpoingiza ndani ya chama watu toka nje ya CCM ambao hata uanachama wao unatia mashaka ( CCM maslahi).
Matokeo yake ni kuwa kadiri siku zinavyoenda, kila chaguzi CCM wanatumia nguvu nyingi sana ili kushinda. Kama sayansi iko sahihi basi hili lina mwisho na huenda tamati iko karibu kuliko tunavyodhani.
 
Makada watiifu na wakongwe, siwaoni kabisa humu naona wale wa kwenye vijiwe vya kahawa tu
 
Yaani ulipoanza kusema habari ya katiba mpya ndo umeanzia pumba hapo. Yaani CCM iangushwe na kelele za katiba mpya?
Thubutu!!!
Watanzania siyo ndondocha kama mnavyodhani. Wanaelewa mno. CCM itang'oka kwa uasi utakaotokea ndani ya CCM,na siyo vinginevyo. Na pia siyo leo wala kesho.

Ishu ya katiba mpya ipo midomoni mwa malofa wachache ambao sikosei nikiongeza,na wapumbavu wachache. Labda Samia alainike tu,vinginevyo hakuna wa kuibabaisha CCM na huo ujinga so calle Katiba mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ccm inaondolewa na nguvu ya umma kwakutupiwa mawe sio muda mrefu utaikumbuka Hii comment yangu
 
Huyu mama ndio ameamua kuichimbia kaburi, tatizo upinzani wapo busy kumsifia as if walimchagua. Siku watakapoungana kama Ile 2010 na 2015 ndio wangeimaliza kabisa hiyo CCM. Huyu mama hakuna kitu.
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Your browser is not able to display this video.
 
Huyu mama ndio ameamua kuichimbia kaburi, tatizo upinzani wapo busy kumsifia as if walimchagua. Siku watakapoungana kama Ile 2010 na 2015 ndio wangeimaliza kabisa hiyo CCM. Huyu mama hakuna kitu.
Sifa hupumbaza na kulevya....!!!!
 
Watashinda kama ambavyo wamekuwa wakishinda.CCM hata ivurugike kiasi gani,hua inajua namna ya kushinda uchaguzi."Siasa ni Sayansi ";Dr.Slaa.
 
Mpaka sasa hakuna upinzani unaoweza kuitoa CCM madarakani. Haupo.
Wewe huelewi maana ya kuitoa CCM madarakani. Unafikiri kuitoa madarakani ni lazima iingie CHADEMA au ACT. Njia rahisi ni wapinzani wengi kuingia CCM na kuchukua uongozi wa chama kisha kuwatupa nje wenye chama. Huko ndiko kuiondoa kisomi. Angalia idadi ya waliotoka CHADEMA na kushika madaraka chamani, bungeni na serikalini huku wakiwaacha wenye chama wakishangaa na kubaki midomo wazi. Muda si mrefu CCM itaongozwa na wapinzani. Rudi darasani kijana ujue maana na mbinu za mapinduzi katika nchi na vyama
 
Inawezekana kweli ccm ni toleo la mwisho lakini upinzani wa kweli upo taabani hospital unatiwa dripu hauna nguvu tena kumuangusha huyu aliebakia mwisho
 
Ona huyu anaota mchana. 😂
 
Inawezekana kweli ccm ni toleo la mwisho lakini upinzani wa kweli upo taabani hospital unatiwa dripu hauna nguvu tena kumuangusha huyu aliebakia mwisho
Inawezekana kweli ukawa sahihi lakini je ndio uhalisia?
 
Kuna immigrants waliokosa teuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…