Haya mambo usijekuingia kichwa kichwa hata ukiona guest house ina restaurant hapo hapo usije kuingia kichwa kichwa kwa kudhani ni bei cheap.
Kuna siku nimetafuta guest ya mtu wa kawaida mitaa ya tegeta kwa ndevu, sasa bodaboda wakaniambia kuna gest ya Sirro mitaa flani wakanipeleka inaitwa Tongori inn, ebwanaeee nilikaa siku Nne pale kwenye room ya 30,000 per day lakini kununua chakula chao niliwakwepa[emoji23][emoji23]
Msosi wa elfu 7 wali na kipaja cha kukua sishibi eti, nilichofanya nikuagiza mitaa ya nje tu kikija cha buku mbili jero simalizi.
Moral of the story: usipende kulazimisha maisha mkuu, ukiona umejikuna mkono haufiki basi lala ila kula nenda kale nje ya hyo hotel fullstop.
Kwa hapo ubungo kama uko majalala kabisa tembea nenda kale CoET UDSM japo ratio ni ndogo ila sio bei ghali unaweza kula hata plate mbili kama ni mpiga menyu sana.[emoji23] [emoji23]