Hii ni halali kweli??

Hii ni halali kweli??

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,497
Reaction score
16,180
Salaam wakuu!
Jana nimelala hotel kubwa tuu pale maeneo ya ubungo, sasa mda flani nikahisi njaa nikasema wacha niagize chochote. Nikachukua kitabu cha menu nikaona tropical fruits =4000tsh sasa nimeagiza nikaletewa kipande cha tikiti na ndizi moja. Wakuu hii sio fair kabisa yaani nimemind kinyama aisee.
 
Kulala tunalala hotelini, kula kwa mama ntilieeee.... Piga wali nazi mixer Amira kwa buku.... Siku tatu husikii njaa.... Sasa wewe hayo mamenyu yako yatakuponza hayo... Dadek.
 
Acha undezi umeshasema hoteli kubwa na mambo take makubwa kama hayo, wenzako wanauziwa ndizi 2 7000 we na tikiti juu unalalamika,
 
Kulala tunalala hotelini, kula kwa mama ntilieeee.... Piga wali nazi mixer Amira kwa buku.... Siku tatu husikii njaa.... Sasa wewe hayo mamenyu yako yatakuponza hayo... Dadek.
Mkuu kwakweli yameniponza
 
Salaam wakuu!
Jana nimelala hotel kubwa tuu pale maeneo ya ubungo, sasa mda flani nikahisi njaa nikasema wacha niagize chochote. Nikachukua kitabu cha menu nikaona tropical fruits =4000tsh sasa nimeagiza nikaletewa kipande cha tikiti na ndizi moja. Wakuu hii sio fair kabisa yaani nimemind kinyama aisee.
alafu huku njee watu wana lalamika vyuma vimekazi ,sijui biashara ngumu vita ya ufisadi ndio hiyo hapo hotelini mtu anataka kupata faida ya ajabu wakati huduma mbovu
 
Hahaha mi siku moja niliagiza ugali yaani niliumega mara mbili tu ukaisha nilimindi kinoma alafu tshs 8000, ilibidi niende zangu nje kutafuta chakula
 
Hahaha mi siku moja niliagiza ugali yaani niliumega mara mbili tu ukaisha nilimindi kinoma alafu tshs 8000, ilibidi niende zangu nje kutafuta chakula
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] ungeomba part two mkuu
 
Ungetoka pale barabarani ungejichagulia tikiti zimazima kwa sh,3000 tu.ndizi ungepata 4 kwa sh.1000.ungemenyewa na ungeweza hata kuwagawia na watu wengine wenye njaa barabarani.saafi.
Lakini sio mbaya ndio raha ya mji wa dar hiyo.
 
Haya mambo usijekuingia kichwa kichwa hata ukiona guest house ina restaurant hapo hapo usije kuingia kichwa kichwa kwa kudhani ni bei cheap.

Kuna siku nimetafuta guest ya mtu wa kawaida mitaa ya tegeta kwa ndevu, sasa bodaboda wakaniambia kuna gest ya Sirro mitaa flani wakanipeleka inaitwa Tongori inn, ebwanaeee nilikaa siku Nne pale kwenye room ya 30,000 per day lakini kununua chakula chao niliwakwepa[emoji23][emoji23]

Msosi wa elfu 7 wali na kipaja cha kukua sishibi eti, nilichofanya nikuagiza mitaa ya nje tu kikija cha buku mbili jero simalizi.

Moral of the story: usipende kulazimisha maisha mkuu, ukiona umejikuna mkono haufiki basi lala ila kula nenda kale nje ya hyo hotel fullstop.

Kwa hapo ubungo kama uko majalala kabisa tembea nenda kale CoET UDSM japo ratio ni ndogo ila sio bei ghali unaweza kula hata plate mbili kama ni mpiga menyu sana.[emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom