Hii ni Hali ya kawaida au Kuna Tatizo sehemu

Godoro la kioo

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2025
Posts
456
Reaction score
1,003
Salam wakuu. Bila kuwachosha

Kuna Hali flani imekuwa ikijirudia Sasa nashindwa kuelewa je ni Hali ya kawaida au dishi lishaanza kuyumba

Yaani Kuna Ile unatembea tembea mara umefika sehemu ukiangalia Yale mazingira na kinachoendelea pale ni kama siyo mageni yaani kama ushawahi kufika hapo kabla na tukio Hilo ushawahi kuliona Tena mazingira hayo hayo

Ila ukijaribu kuvuta kumbukumbu unaona kama vile hujawahi kufika hiyo sehem

Sasa nauliza hii ni Hali ya kawaida na je Kuna yeyote imewahi kumtokea
 
N
Network zinaanza kupungua Strength braza nenda hospitali
 
Yaani Kuna Ile unatembea tembea mara umefika sehemu ukiangalia Yale mazingira na kinachoendelea pale ni kama siyo mageni yaani kama ushawahi kufika hapo kabla na tukio Hilo ushawahi kuliona Tena mazingira hayo hayo
Sahihi
 
Ata Mimi Huwa inanikuta Hali hiyo kama yako naona kama mazingira nishafikaga
 
Mimi na tatizo la kukutana na watu tunakuwa km tunafahamiana sana ila mimi huwa siwakumbuki

Au kufananishwa na mtu
Yote kwa pamoja yanawezekana labda wanakujua ila huwakumbuki au wanakufananisha
 
Hiyo sehemu unakuwa ulishafika kiroho(Nafsi yako ilishawahi kufika i.e ndotoni nafsi ndio huwa kwenye tukio so nafsi yako itakuwa ilishafika hapo).
Relax ni kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…