Hapana.
Siyo kwa sababu ya Katiba tu; ni kwa sababu ya tabia za watu (raia) zilivyo geuzwa na kuwa za kushangaza kabisa.
Ndiyo.
Kwa jinsi nchi hii raia walivyo sasa hivi hilo ni rahisi kabisa kwa mtu kama huyo kutamka na likafanyika kweli; kwa sababu hakuna chombo/kundi linalo weza kuhoji anachofanya huyu mtu mmoja. Lakini siyo kwa sababu ya Katiba, ni kwa sababu ya watu kutojali lolote linalofanyika ndani ya nchi hii.
Kwa mfano: tendo la watu kutekwa na kupotezwa tu hivi hivi, na likaonekana sasa kuwa ni jambo la kawaida tu?