Hii ni kazi kweli au mi ndo kazi?

Lunovar

Member
Joined
Mar 26, 2022
Posts
11
Reaction score
31
Nipo kwenye group fulani hivi la WhatsApp likatumwa tangazo la ajira kutoka Pepsi (nimeambatanisha hapo) lilikua linahitaji vijana wa kuwaajiri na mimi nikajaribu kuomba hapo baada ya siku kadhaa wakanijibu hivyo(nimeambatanisha pia).

Watu mliopata bahati ya kuajiliwa kwenye makampuni makubwa au wenye uzoefu na mambo ya ajira, naomba kufahamu hii ni kweli au ni matapeli?

 
huo utapeli hilo tangazo ni fake wanataka tu utume hiyo ela utapelewe
 
Utapeli huo huyo Said Abdallah hata kuandika hajui, eti gharaza za chakula badala ya gharama za chakula. Halamu hicho cheo ni Country Manager au County Manager ?πŸ™„
 
Hapa WEWE NDO KAZI mkuu. Jichanganye sasa ULIWE kimasihara.
 
Picha Lina anza Pepsi Wana tumia Gmail (πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜πŸ˜)
Halafu mhuri sasa miksa Said abdalah et ndo kantri meneja Mzee kama ni Fresher ukienda kimhemko utaliwa
Matapeli hayo kimbia πŸƒπŸƒ
 
Tangazo ni fake, mhuri fake, hakuna mtu aliyewahi kulipia malazi ya usahili(utapigwa ulie kenge) na zaidi SBC hawaajiri watu wengi hivyo
 
Hapo wewe ndio kazi mzee wangu.
Hilo tangazo Pepsi walishaga likana kuwa sio la kwao.
 
Uliona wapi kampuni kubwa zinatumia email za Gmail? Ambazo hata wewe unaweza kufungua?

Watu wako desperate sana na ajira na fursa ndio wewe!

Kampuni zote hutumia email za za website zao, data zinakuwa stored kwenye sever zao sio Gmail eg. Info@Sbc.com ,info@cocacola.com

Gmail wanakuvuta chumbani! Stuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…