- Thread starter
- #21
Raha yoote iko kwenye makeup! Yaani kuna saa unatamani ugomvi ili mpatane. Raha yake ukute anaejua kumbembeleza. Kama wewe hujui kubembeleza usimtese mtoto wa watu, muache aende zake.
Itabidi unipe siri zaidi ya mazingira yanayokupelekea utamani ugomvi na ni vipi unabembelezwa mpaka mnarudi kwenye hali ya kawaida. Ila hata kama hiyo ni sababu ya kweli sidhani kama utakuwa unahitaji ugomvi wa mara kwa mara ili tu ubembelezwe. Inakuwa "monotonous" na kumbuka kila ugomvi una madhara yake kwenye mahusiano na ukilimbikizwa matokeo yake yanaishia kuwa makubwa yasiyorekebishika.