Hii ni kwa akina dada tu

Hii ni kwa akina dada tu

Raha yoote iko kwenye makeup! Yaani kuna saa unatamani ugomvi ili mpatane. Raha yake ukute anaejua kumbembeleza. Kama wewe hujui kubembeleza usimtese mtoto wa watu, muache aende zake.

Itabidi unipe siri zaidi ya mazingira yanayokupelekea utamani ugomvi na ni vipi unabembelezwa mpaka mnarudi kwenye hali ya kawaida. Ila hata kama hiyo ni sababu ya kweli sidhani kama utakuwa unahitaji ugomvi wa mara kwa mara ili tu ubembelezwe. Inakuwa "monotonous" na kumbuka kila ugomvi una madhara yake kwenye mahusiano na ukilimbikizwa matokeo yake yanaishia kuwa makubwa yasiyorekebishika.
 
kwa umri huo wa 37years ni hormonal changes anelekea kwenye menopause kaka
so takecare.

Mkuu nilikuwa sijui kumbe kuna wanaume nao wanaingia kwenye menopause? Mimi nilidhani ni mambo ya kinamama hayo. Huyu wa 37 atakuwa na matatizo binafsi kwani hata kile kipindi cha mid-life crisis kinachowakumba wanaume hajakifikia.
 
kudeka.com! Kama mwanaume hajui kubembeleza inakuwa kununiana.com! Ila kununa c vzur wadada! Tuwe wawaz kama m2 kakukera unamwambia hakuelew bora ugeuke mzungu unampa vbao vya shav vwil! Mwenyew atajbeba mbele ya safar!

uwiii....vibao hapana....nitajikuta utumbo nje ndani....hii waachiwe wazungu wenyewe....mswahili atakuuwa.....
 
huwa tunaona tumewakomesha sana....na ukibembeleza basi roho kwatuu....yaani burudani....
ila ongea nae mwambie hupendi.....

Uzire bila sababu halafu nikubembeleze....!To hell. . . !!!!!!!!
 
mie huwa nazira/susa hasa kama ninataka kumpiga mzinga
 
Jamani samahanini mimi sio mdada napita tu, umbea huo! Msituchunie hivyo jamani, pia msijadili sana hili sababu lipo mahakamani ...
 
Honestly hii tabia ya kuzira sijui kununa hua inanikera! Eti unakuta jianaume zima linanuna kwa sababu ya kitu kidogo tu khaaa! Mi hua siwezi kucope na watu wanaonuna hovyo!
 
Tata binafsi huwa sioni kama hili ni tatizo sana kwani kuzira ni tabia aliyonayo binadamu kuonyeha hajaridhika/hajafurahishwa na jambo au kitu fulani. Tofauti ni namna ya kui-express na ku-deal nayo. Na hii haiko kwenye mapenzi tu, hata madaktari walizira

Kwangu mimi njia nzuri ya kuiepusha kuzira ni ku-deal na source (mara nyingi ni maudhi), wala siyo kumkaripia eti kwa kuwa amezira ili hali ana-express dissatisfaction yake!

Oooho! kumbe uliuliza kina dada tu, samahani sikusoma vizuri nikajikuta nimeishaandika!

Usitie shaka bado unakaribishwa kama mdau/mtazamaji - una-comment pale tu uzalendo unapokuzidia.
 
Tabia hii ina ni kera sana

Waitu rutta punguza jazba. Huu ni uwanja wa watani wa jadi kutueleza ni nini hasa kinawasukuma kususa hata yale mambo yetu ya msingi. Ukileta jazba hapa watasusa kuchangia hii thread.
 
Mkuu nilikuwa sijui kumbe kuna wanaume nao wanaingia kwenye menopause? Mimi nilidhani ni mambo ya kinamama hayo. Huyu wa 37 atakuwa na matatizo binafsi kwani hata kile kipindi cha mid-life crisis kinachowakumba wanaume hajakifikia.

Ndugu angekuwa mwanaume swali lisingeulizwa wakina dada
muhusika ni mwanamke na muuliza swali ni mwanaume kwa uelewa wangu
i stand to be corrected if i'm wrong.
 
Mimi wife akizira na mie huwa nazira...mwiho wa siku analegeza mwenyewe.... si unajua tena hawa viumbe walivyo laini
 
Mimi wife akizira na mie huwa nazira...mwiho wa siku analegeza mwenyewe.... si unajua tena hawa viumbe walivyo laini

Kwa wastani huwa analegeza msimamo baada ya muda gani ndugu yangu?
 
NIKILIA nabembelezwa kwa upendoo.

Na hata ni NIKINUNA nabembelezwa kwa upendoo.

Na hata NIKISUSA nabembelezwa kwa upendoo.

Je wewe hujawah kubembelezwaa, je wewe hujawahi kubembelezaaa
 
Back
Top Bottom