Sijui sana kuhusu hiyo chaguzi draw cap maana si mtaalamu sana wa kubeti japo nimemuelewa mdau aliyenielewesha kuihusu hapo juu.
Ila kama ingekuwa unahitaji kubashiri Yale matokeo matatu tu(nyumbani,ugenini na sare) ingekuwa hivi;
Mechi ya kwanza ikiisha matokeo yanayowezekana ni ya aina tatu.Mfano kuna mechi kati ya Arsenal na Tottenham.Hapo chaguzi zilizopo ni Arsenal win/Tot lose,Draw na Arsenal lose/Tot win.
Sasa chukulia unataka ubashiri mechi mbili;
Arsenal vs Liverpool na Tottenham vs Chelsea. Chaguzi zitakuwa hivi;
Mkeka wa 1,Ars win & Tot win. Wa 2,Ars draw & Tot draw. Wa 3,Ars lose&Tot lose. Wa 4,Ars win & Tot lose. Wa 5,Ars lose & Tot win. Wa 6,Ars draw & Tot lose. Wa 7,Ars draw & Tot win. Wa 8,Ars win & Tot draw. Wa 9,Ars lose & Tot draw.
Kwa hiyo kama unavyoona kwa mechi moja ili ujihakikishie ushindi wa kula mkeka mmoja ni lazima ubashiri mikeka mitatu.Kwa mechi mbili ili ujihakikishie ushindi wa mkeka mmoja lazima ubashiri mikeka tisa.Hivyo formula ipo hivi;
Mechi moja=3¹=3.
Mechi mbili=3²=9.
Mechi tano=3^5=243.
Hivyo yafaa ubashiri mikeka 243!
242 lazima ichanike na mmoja lazima ule.