Hii si kweli hata kidogo. Tamasha hii ilipangwa na Bob Astles. Astles alikuwa Mwingereza aliyebaki Uganda baada ya ukoloni akashiriki na serikali ya Obote na kuendesha biashara zake. Alimwoa Mganda kutoka ukoo wa kifalme. Alikuwa na shamba la mananasi. Amin aliposhika utawala 1971 akamtupa gerezani, akamwachisha baadaye. 1975 Amin alimtaka mshauri kwa mawasiliano na nchi za nje akamchagua Astles. Astles alijitahidi sana kumbembeleza Amin kwa kila namna.
Wakati Amin alichaguliwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (aibu juu ya madikteta wote wa Afrika waliompa kura!) kulikuwa na party. Kwenye nafasi hii Astles alitisha wafanyabiashara Waingereza walioishi Uganda wambebe Amin mbele ya wageni wa Umoja wa Afrika. Baadaye aliamuru idadi ya Waingereza waliokuwa wafanyabiashara Uganda wapige magoti mbele ya Amin. (kwa nini waliitikia? ).
Astles alikuwa hodari kumbembeleza Amin. Alihukumiwa naye hadi mauti mara nne lakini alifaulu kila safari kumbembeleza tena. Baada ya uvamizi wa Tanzania pale Uganda na kurudishwa kwa Obote Astles alitupwa tena jela kwa miaka 4 au 5, hatimaye aliachishwa akarudi Uingereza....
Kuhusu siku zile ambako Astles alipowalazimisha Waingereza wenzake kumbeba Amin, askofu Mwanglikana Mganda Festo Kivengere aliandika: "At the very moment the heads of state were meeting in the conference hall, talking about the lack of human rights in southern Africa, three blocks away, in Amin torture chambers, my countrymen's heads were being smashed with sledge hammers and their legs being chopped off with axes."
Bado unataka kusheherekea picha hii???
(halafu: si kweli Waingereza hawataki kuona picha hii jinsi unavyodai kwenye kichwa cha habari. Bila shaka ilionyeshwa zaidi huko kuliko Tanzania)