POTOSHI Hii ni picha ya wagonjwa waliolala chini ni kweli imepigwa katika hospitali ya Kyela?

POTOSHI Hii ni picha ya wagonjwa waliolala chini ni kweli imepigwa katika hospitali ya Kyela?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimekutana na hii taarifa huko Facebook kwa huyu mdao Kyela Tz anaeleza kuwa hii ni picha ya wagonjwa katika hospital ya wilaya ya Kyela wakiwa wamelala chini.

Wafungwa.jpg
 
Tunachokijua
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook amechapisha baadhi ya picha zinazoonesha watu wakiwa wamelala chini na wengine wameketi wakiwa wamesngamana na kueleza kuwa ni hali iliyopo katika hospitali ya wilaya ya Kyela.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa madai yaliyowekwa hayahusiana na picha zilizoambatanishwa na hivyo kupotosha.

Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo Google reverse image search, JamiiCheck imebaini kuwa picha hizo hazijapigwa nchini Tanzania na badala zimepigwa kutoka katika maeneo mengine nje ya Tanzania.

Miongoni mwa picha hizo inayowaonesha watu wakiwa wamelala chini ilichapishwa mwaka 2016 mtandaoni na tovuti ya Modern Ghana ikihusiana na taarifa ya wafungwa katika nchi hiyo. Taarifa hiyo iliyoambatanishwa na picha hiyo inaelezea namna gani wafungwa nchini Ghana walivyokuwa wanalalamika baada ya wenzao kufia gerezani na kuomba kuwa magerza yanapaswa kuwasahihisha na siyo kuwaua.

Picha nyingine pia inayowaonesha watu wakiwa wamekaa imekuwepo mtandaoni kwa kipindi kirefu kuanzia 2016 ikirejelea wafungwa wakiwa katika gereza, picha hiyo imtumika na vyanzo mbalimbali ikiwemo vya Nigeria na Ghana kurejelea hali ya magereza na wafungwa katika mataifa hayo. Mathalani rejea hapa, hapa, hapa, hapa, hapa.
Nyumbu ukute wameshasambaziana sana kwenye magurupu yao ya wasap na insta
 
Back
Top Bottom