Wakuu,
Haki nacheka kama mazuri



, mara hii mmeshasahau yote yaliyotokea? Aaah bana mbona mnataka kutupa mpira mapema hivi?
Sasa hivi mtakuwa mnalia na kusaga meno huko mliko, yaani wote ambao mngewaangushia lawama mliwapiga ban, sasa hakuna mtu wa kumtupia mzigo! Mnaogopa kuwaangushia lawama polisi maana nao watamwaga mboga. Aaaah tumefikia kutamu sana.
Aliyetoa mchongo wa kufungia CHADEMA kufanya siasa atakuwa anasaga meno huko aliko. Watu wana Mungu bwana.... kama alivyosema Ruge ogopa Mungu na Teknolojia, sisi wala hatuna haraka, tunaendelea kufuatilia episodes tukiwa tunatafuna karanga na bisi.... ni humu tuuu!😎
CCM mko na vyote isipokuwa akili tu🤣🤣, msuka mipango, anayewafuata, anayetekeleza, anayekuja kutupigia kelele wote mmejaa funza vichwani! Hakuna kitu mmewahi fanya kikaenda vizuiri, ni failure after failure, poor poor kwa sauti ya Steve Nyerere, au nakosea guys?
Dr. Mwigulu Nchemba



====
View attachment 3576373
"Watanzania, leo tumekuja na jambo moja tunaomba sana mtusikilize.
Siku ya tarehe 29 tulikubaliana na Chadema kwamba twende tukafanye vurugu tutalipwa. Lakini pia Chadema ilituambia kwamba tutaungana na Jeshi la Tanzania.
Sasa kitendo kilichotuuma ni kwamba tulitoka tarehe 29 kufanya vurugu, lakini hakuna jeshi lililotuunga mkono. Wengine tukaambulia kuumia tu, lakini hicho kitendo hakijatuuma sana.
Kilichotuuma ni serikali ya Chadema kututelekeza, kutuacha tunahangaika. Tulikubaliana twende tukapindue serikali ya Samia kwamba tutapata haki zetu, tutalipwa zote kwa pamoja.
Lakini cha ajabu, tumepata wageni wengine kutoka Kenya wamekuja, wamelipwa hela zao wao. Lakini sisi vijana wa Tanzania tumebaki tunahangaika hatujui tukae wapi, hatujui tujifiche wapi.
Kwahiyo tulikuwa tunaiomba serikali kwanza ya Tanzania itusamehe makosa yetu kwa sababu tulikuwa..."