Nimekubali masahishisho haya.
Nimekubali masahishisho haya.
Thuweini Ally aliingia Simba 1979, ikiundwa na vijana wengi wakiwa shule:Umiseta, baada ya wakongwe wengi kuondoka, akabaki Marehemu Omari Mahadhi; Daudi Salum; na Marehemu Kajole. Coach akiwa ...Willy Mwaijibe. I think alitokea Kikwajuni. Alikuwa akifunga kila mechi.
Simba ya vijana wale akina Filbert Rubibira, Hussein Tindwa (Alifia uwanjani mechi ya Racca Rovers), Abbas Kuka, George (Best) Kulagwa, Nicodemus Njohole, Thuweini Ally, Rahim Lumelezi na Martin Kikwa ndiyo ilifungwa 4-0 na kurudisha 5-0 Zambia. Nafikiri kwenye 5-0, Thuweini alifunga goli/magoli.
Peter Tino akiwa amemaliza form 4 na akiwa star wa umiseta na kina Njohole, Peter Muhina e.t.c ndiyo alienda Taifa Stars.
Kwa kuwa Yanga ilikuwa na hali ngumu baada ya mastaa wake kuunda Pan, Simba na Pan ndiyo walikuwa mahasimu wapya, ingawa sikumbuki kama Pan iliwahi kuifunga Simba.
Akina Adolph;Mkwenche;Gordian;Pondamali na wengineo wa Pan: Yanga Kids na B ya zamani ndiyo walikuwa mahasimu wapya wakipambana na akina Nico, George Kulagwa waliokuwa awali Simba B na wengine wageni.
Kwa record: Wakati Tanzania inashiriki fainali ya 1980, Leodgard Tenga alikuwa ameisha maliza Chuo: 1978, unless kwa sababu zingine. Aliacha mpira baada ya fainali, zaidi kwa sababu za kitaaluma/kikazi baada ya kuhitimu chuo.
Peter Tino, anaenziwa kwa ajili ya impact ya goli lake. Wangebadilishana na Adolph, yeye akafunga Dar, Adolph Zambia, Adolph ndiyo angeenziwa. Dynamics za mashindano, uwezo wa kuleta mabadiliko wakati ambao ungeweza kukata tamaa au kuharibu kwa kukosa uangalifu hatimaye kutoka na matokeo ya mwisho, ndipo kwenye heshima, ingawa kiujumla wote wanastahili pongezi.
Tuulizane, mechi ya juzi TZ-UGANDA, aenziwe nani? mmoja tu!