Kilwa mji wa Kale mfano wake kulikuwa na majengo yenye vyoo na yamekuja kuvunjwa na Mreno kwa mizinga hadi leo magofu yake yana sehemu ya choo.
Timbuktu kulikuwa na maendeleo makubwa karne ya 11 hata kabla ya hiyo Nyumba haijajengwa. Watu walimiliki vyoo, na majengo ya kila namna. Hadi kulikuwa na chuo kikuu Timbuktu.
Afrika ya magharibi kulikuwa na kiwanda kikubwa cha nguo chenye nguvu kuliko cha Manchester England.
Waliyosema Afrika ilikuwa sawa hawakusosea ni kweli, ila mambo yalibadilika kuanzia karne ya 15 walipoanza kumiminika wageni kutoka mataifa mbalimbali. Hao ndiyo waliharibu kila kitu na hata kuvunja majengo mengine ya kale. Ndiyo maana vitu vingine ushahidi hakuna kwasababu waliharibu kusudi. Mfano Kilwa kuvunjwa dola iliyoendelea hadi kumiliki sarafu yake, hivi sasa ni magofu tu