Naomba kuuliza wataalamu wa ujenzi hizi nyumba za hivi (kama zinavyoonekana sio kubwa) zinaweza kufikia gharama za ujenzi na finishing kali kiasi gani? nataka nikiwa na pesa kamili au inayokaribia kumaliza nyumba ndo nijenge, vyumba viwili au vitatu vidogo na bati llitolee maji nyuma hiyo hidden roof iwe mbele tuu. Msaada wenu tafadhali 😊
Hiyo nyumba ni ya kisasa. Na finishing yake Inaitwa primier finishing. Inawez ika gharimu Zaid ya million 100 na kuendelea. Na kama Hauna experience na ujenz kbs bs utataboka sana
Watu wengi wanatoa lawama kwenda Kwa fundi kupaua.
Ila nyumba za hidden roof wa kulaumiwa si fundi bati pekee.
Tatizo la msingi linaanzia kwenye mchoro mzima wa nyumba kabla hata ya kujegwa.
Kuna sehemu niliitwa kwenda kurekebisha nikakuta PVC ya nchi 4 ndiyo imewekwa kama mfereji wa kupokea maji yote ya paa zote mbili 🤔
Matokeo yake mvua kidogo mferji unafurika maji