Hii picha Ina tatizo gani

Hii picha Ina tatizo gani

Msumb

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
3,452
Reaction score
5,372
Imepostiwa na Page ya club ya Al Ahly katika kurasa zao je? Ina shida Gani!
20240329_080347.jpg
 
Kama ulisikia kisa cha shabiki wa Algeria aliyefukuzwa Nchin I Cory coast basi hoja ya Al ahly ipo hapo.
 
Haina matatizo yoyote
Wamepost uwanja ulivyo nje na ulivyo ndani
 
Nilivyowaza lengo Lao ni kuonesha namna gani tulivyokithiri kwenye umasikini wa kutupwa
Kwenye majiji yote ya Tz kuna Slums kama hizo.

Serikali inabidi ije na mpango wa kuziondoa na kuruhusu wawekezaji wajenge majengo mazuri
 
Lango kuu la nchi limezungukwa na slums. Umasikini.
 
Ukitembea nchi za watu kisha ukaja Tanzania ukajiuliza sisi ni masikini hadi akili.

Uwanja wa Taifa umezungukwa na mabanda umiza, nyumba zisizo na hadhi kukaa mjini.
Kulikuwa na haja Serikali ikaenda kuzinunua hizo nyumba KUU KUU kisha kujenga za Kisasa walau kuupa hadhi uwanja wetu wa Taifa

Aibu nyingine ni za kujitakia 🙌
 
Kwenye majiji yote ya Tz **** Slums kama hizo.

Serikali inabidi ije na mpango wa kuziondoa na kuruhusu wawekezaji wajenge majengo mazuri
Wawekezaji wanadai wananchi wamekua jeuri na wananchi wanadai wawekezaji ndo viburi. Hapa wanashindwana kwenye thamani ya viwanja
 
Wawekezaji wanadai wananchi wamekua jeuri na wananchi wanadai wawekezaji ndo viburi. Hapa wanashindwana kwenye thamani ya viwanja
Hahahaaa, hapo kweli lazima watataka kupewa cha juuu
 
Kwa walioko mikoani kununua kibanda kibovu/ kiwanja chenye kibanda/nyumba mnazoziona hapo miguu ishirini kwa ishirini haipungui milioni 100!
 
images (54).jpeg
akili ndogo za kitanzania zitahisi lengo la ahly nikutudhihaki, lahasha. Wao wamepiga picha ya umbali hata watanzania huwa tunapiga.
Egypt kuna maeneo dhohofu kushinda hapo,
Kuna eneo kama kimara lote hamna nyumba iliyopigwa rangi bali tofali za kuchoma. Though hatufurahii umaskini.
 
Acheni kujihisi, kujishtukia na kujishusha.... kwanini umefikiri wamemaanisha tatizo?
 
Back
Top Bottom