SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kabla ya kuisha mwa msimu wa 2022-2023 nilikuja na mkeka ulioelezea jinsi Simba inavyotakiwa kubadilisha kikosi chake kwa mtiririko fulani wa kuacha wachezaji ili ndani ya misimu 3 ijayo iwe na kikosi kipya kabisa.
Lilipokuja dirisha kubwa la usajili, mkeka wangu ulionekana kufuatwa kwa 95% kama si zaidi. Kosa kubwa lililofanyika katika msimu hii miwili ni aina ya wachezaji walioletwa kama maingizo mapya kutokidhi viwango vilivyotegemewa.
Saidoo pamoja na kile kinachoonekana mchango wake ndani ya Simba hakuwa ingizo sahihi katika timu. Bado naamini ni mmoja wa wachezaji waliochangia Simba kufanya vibaya kwa misimu hii miwili. Sijui ni akili gani zilitumika kuleta mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi ya yule unayekuja kumreplace ndiyo awe mbadala wake.
Katika uzi ule nakumbuka kusema Chama ana misimu 3 tu ya kuitumikia Simba katika kiwango cha kuridhisha, baada ya hapo anatakiwa awe mchezaji wa kutokea benchi kama ataendelea kusalia ndani ya Simba. Leo ni rasmi Chama hayupo tena chamani. Hili ni jambo jema.
Hii safisha safisha inatakiwa iwafikie pia viongozi mamluki wanaotumiwa na wale wasioitakia mema Simba, wanaoivuruga na kuwarubuni wachezaji. Bila kufanya hivyo maingizo mapya nayo yatageuzwa maduka na vivuruge kama hawa wanaotoka.