Hii safisha-safisha inayoendelea ndani ya Simba inapendeza sana

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kabla ya kuisha mwa msimu wa 2022-2023 nilikuja na mkeka ulioelezea jinsi Simba inavyotakiwa kubadilisha kikosi chake kwa mtiririko fulani wa kuacha wachezaji ili ndani ya misimu 3 ijayo iwe na kikosi kipya kabisa.

Lilipokuja dirisha kubwa la usajili, mkeka wangu ulionekana kufuatwa kwa 95% kama si zaidi. Kosa kubwa lililofanyika katika msimu hii miwili ni aina ya wachezaji walioletwa kama maingizo mapya kutokidhi viwango vilivyotegemewa.

Saidoo pamoja na kile kinachoonekana mchango wake ndani ya Simba hakuwa ingizo sahihi katika timu. Bado naamini ni mmoja wa wachezaji waliochangia Simba kufanya vibaya kwa misimu hii miwili. Sijui ni akili gani zilitumika kuleta mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi ya yule unayekuja kumreplace ndiyo awe mbadala wake.

Katika uzi ule nakumbuka kusema Chama ana misimu 3 tu ya kuitumikia Simba katika kiwango cha kuridhisha, baada ya hapo anatakiwa awe mchezaji wa kutokea benchi kama ataendelea kusalia ndani ya Simba. Leo ni rasmi Chama hayupo tena chamani. Hili ni jambo jema.

Hii safisha safisha inatakiwa iwafikie pia viongozi mamluki wanaotumiwa na wale wasioitakia mema Simba, wanaoivuruga na kuwarubuni wachezaji. Bila kufanya hivyo maingizo mapya nayo yatageuzwa maduka na vivuruge kama hawa wanaotoka.
 
Post yenyewe wenye mkeka ni hii hapa.

 
Uko wapi huo uzi wenye mkeka?
 
Huko wanaacha vile vile yaan una safisha nje Ila ndani unajaza matakataka unategemea nini? Hali itabakia kua vile vile tu Simba inaenda kugeuka Ashanti United
Hahahahaha...baadae waje kulalamika humu viongozi hawafai
 
Kwa hiyo kila msimu mtakuwa kazi yenu ni kusafisha tu! Kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi!! Halafu mwisho wa siku mnaishia kushika nafasi ya pili/tatu kwenye msimamo wa ligi kuu!!
 
Eti viongozi wanaotumiwa kuisaliti simba !!! Acheni sababu zisizo mashiko
 
Nawapongeza sana viongozi kwa maamuzi sahihi.
Chama aliifanya Simba kama duka lake.Mechi zote muhimu kwa Simba za hapa ndani alicheza chini ya kiwango.Hii haikuwa bahati mbaya.
Yanga wanajua kiwango cha chama hakijawahi kushukuka ila pesa yao ilikishusha ili wanufaike na udhaifu wa Simba
 
Hayo mabaki huwa yana sehemu yake maalumu pale utopoloni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…