Hii sasa imekuwa kero! TRA, chukueni hatua kurekebisha tatizo la taarifa za marejesho mtandaoni (e-Filling Returns)

Hii sasa imekuwa kero! TRA, chukueni hatua kurekebisha tatizo la taarifa za marejesho mtandaoni (e-Filling Returns)

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
2,348
Reaction score
3,038
Jamani watu wa mamlaka tafadhalini hebu chukueni hatua za makusudi kurekebisha hili tatizo la taarifa za marejesho mtandaoni (e-Filling Returns)

Kusema ukweli imekuwa kero isiyovumilika tena, inapofika tarehe za marejesho mtandao unazidiwa inaweza kuchukua zaidi ya siku moja mpaka 5 pengine mpaka siku 7 kufaili return moja aidha iwe VAT au PAYE au SDL

Inafikia wakati kila unapojaribu kuingia mtandao unakutoa, Ndugu zangu kama tumeamua kwenda kidijitali basi tukubali kuwekeza kidigitali kinyume na hivyo inageuka kuwa mateso kwa wafanya biashara hasa sisi waganga njaa wa biashara ndogondogo na internet zetu za kuunga unga bando kwenye simu.

Tunaomba mamlaka iwekeze kwenye mtandao kwa sababu hili sasa limegeuka kuwa KERO na USUMBUFU mkubwa sana. Jamani kama bado hatujajipanga basi turudi nyuma kwanza tujipange upya.

Kibaya zaidi inapopelekea umechelewa kufaili return kutokana na mtandao kutokuwa rafiki unapewa adhabu ya kulipa kwa ucheleweshaji wa marejesho, hii sio sawa huu ni usumbufu na uonevu juu.
 
Kwenye mtandao traffic ikiwa kubwa,huleta majanga

Ova
 
Hakuna forum ya kuzungumzia matatizo ya ulipaji kodi za ndani kama ilivyo kodi za forodha. Kimsingi mfumo wa efilling ni wa ovyo. Unafanya kazi polepole sana. Wao wanaona sawa tu. Nilidhani mimi tu. Kumbe tuko wengi.
 
Back
Top Bottom