Hii sasa ni aibu kwa Israel

Hii sasa ni aibu kwa Israel

Kavimbe

Member
Joined
May 9, 2023
Posts
51
Reaction score
80
Mwezi mmoja sasa tokea Israel inaaze kuitwanga Gaza. Israel inaitwanga Ghaza baada ya HAMASI kuishambulia Israel kwa kushitukiza na kuwachukua watu kama Mateka. Lengo la Israel kuibomoa Ghaza ni kutaka kuwachukua Mateka wao.

Israel ni nchi inayoelezwa kuwa inaongoza Ulimwenguni kwa kuwa na Jeshi la kisasa, wakomandoo wa kisasa, waatalamu wa kila aina katika mambo ya Ulinzi na kujihami.

Suali linaloulizwa ni kwanini Israel inachukua zaidi ya mwezi mmoja kuwakomboa mateka wake?

Ni kwanini Israel waporomoshe maghorofa na kuua mawili wa watoto na wanawake badala ya kutumia utaalamu wa kikomandoo kuokoa mateka wao?

Hivi sasa tayari Israel imeizunguka Ghaza yote ni kwanini wasiwanyakuwe mateka wao mara moja.

Badala yake wanasema wataendelea kuua watoto na wanawake mpaka pale Hamasa itakapo waacha huru mateka.
 
Back
Top Bottom