econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Niwe mkweli serikali ya CCM Chini ya Rais Samiah imefeli kwenye suala la Usalama kabisa. Kwa Sasa inteligensia ya Polisi ipo Chini kabisa. Uhalifu unafanyika na Wala polisi hawana taarifa ya uhalifu huo na hata ukiwapelekea taarifa hawaufanyii kazi.
Kwa mfano kifo Cha Samwaja huko Singida. Mtu anatekwa mpaka kuuawa polisi hawashtuki mpaka taarifa zitoke kwenye mtandao ndio wanaanza kuchukua hatua. Au Binti kubakwa na watu SITA bila polisi kugundua mpaka wananchi walipotoa taarifa mitandaoni kuhusu unyama ndipo polisi wakaanza upelelezi.
Kuna taarifa imeibuka ya kwamba ndugu Gerald Ibrahim mkazi wa Uvunza ametekwa na watu wasiojulikana na haijulikani yupo wapi maana hayupo kwenye custody ya polisi. Hii sio sawa , kazi ya polisi ni kulinda raia na Mali zake na sio kuwaumiza kwa ujinga wanazofanya .
Cha kusikitisha zaidi, Kuna watu wanatumia Ikulu kutapeli watu lakini polisi ipo kimya bila kuchukua hatua . Ni muda Sasa Polisi ifanye kazi yake, la sivyo Kuna watu watapata mwanya na kufanya uhalifu usipiopimika na ambao utashangaza watu wengi, Kama ilivyofanyika nchini Kenya kana shakahola au mauaji ya kawangware.
Jeshi la polisi mna nafasi ya kujirekebisha kabla hii Hali haijazoeleka na kuonekana ya kawaida.