Uchaguzi 2020 Hii shamrashamra mwishoni mwa hotuba ya Salimu Mwalimu inasisimua sana

Uchaguzi 2020 Hii shamrashamra mwishoni mwa hotuba ya Salimu Mwalimu inasisimua sana

Ukiona watu walivyofurahi mwishoni mwa hotuba ya Mgombea mwenza wa Nafasi ya urais kwa tiketi ya CHADEMA unapata hisia za matumaini ya ukombozi wa watu toka makucha ya CCM.

Hii mikutano inatuma ujume mkubwa kwa wakalia viti,watu wanazitaka haki zao,na hao wanaodhani kuwa wamesimama waangalie wasije kuwa wameanguka siku nyingi ila hawajitambui.
 
Nilizaliwa miaka mingi iliyopita. Nikakutana na amani, furaha na upendo. Mbona kadri siku zinasogea hivi vitu adimu vinapotea? Ninasikitika sana. Halafu ukiwa mkweli watakuita mpinzani. Haya yalinikuta mwaka 2015 nilichukia sana wizi na ufisadi ulioimaliza nchi kiasi kwamba nilitamani upinzani uchukue nchi.

Ni kwa vile sina influence ya siasa na kwenye chama changu nami ningehama kama walivyohama vingunge. Nilibaki tu kushabikia kama wenzangu walivyokuwa wanashabikia. Nikashtukia naitwa mpinzani tena Chadema wakati hata sijawahi kuwa hata na ukaribu na wanachadema wenyewe na isitoshe toka nizaliwe sijawahi hata kuhudhuria mkutano wachama chochote japo nina kadi ya chama tokaJuly 1990.

Mimi nikiona mambo ya uonevu na wizi huwa ninachukizwa sana. Na nikuhakikishie kitendo cha kudhamiria kabisa kumuua Lissu kilinisikitisha sana. Hatakama angekuwa na kosa gani lakini hiyo ni mtanzania mwenzetu. Na huwa mimi siyo mpiga kura na kura ya kwanza nilipiga 2015 na ya pili nitapiga 2020 baada ya hapo nitaendelea na UTARATIBU wangu wa kutopiga kura. Nitaendelea kutumikia watanzania wote popote pale nitakapokuwa.

Naumia sana moyoni mwangu.
 
Kweli ilani ya : Uhuru , Haki na Maendeleo ya Watu imepita

Wallahi mwaka huu lazima chama kongwe kilicho jibrandi CCM Mpya kinakwenda na kimbunga.

Haijawahi kutokea kila kona ya Tanzania sasa wanataka mabadiliko.

Inshaallah Mwenyezi awawezeshe 28 October wadamke na kwenda mapema kabisa kukiondoa chama kongwe kwa kura za kimbunga.

Wenzetu hawa wa Kusini tayari wameamua

Freedom is coming! 2020
 
Hata Mbeya mlisema hivyo lakini alipotua mwamba huko mkapoteana
unaijua juhudi iliyofanyika kuukusanya huo umati wa mzee baba,penye ukweli tuukubari tu kuwa hawa jamaa 1. hawasombi mtu 2.watu wanawafuata,kuwasubiri hadi usiku. 3. baada ya mikutano wanawapa na pesa za kuwawezesha kusonga mbele.
kwako wewe haya yana maana ipi?
 
Dah maneno mazito haya yenye ukweli mchungu kwa wana-mtaa wa Lumumba kuwa wananchi wameamua sasa basi 2020 !

Babu yangu amenisimulia kuwa hivi hivi michango midogo midogo ya wananchi ndani ya "kapu la ukili " lilozungushwa kila baada ya mikutano ndiyo ilifanikisha Nyerere na timu yake kusonga mbele na kampeni na hatimaye Tanganyika kupata uhuru toka kwa mkoloni.
 
4. Hawana fiesta.
 
Nachingwea wamenifurahisha sana, sichoki kuwatazama.
 
Dah mpaka Nachingwea nanayoijua imekuwa hivi aiseee?

Dah mtihani sana.

Nachingwea kwa ninavyofahamu ni katika ngome kubwa ya CCM mpaka Jakaya mwemyewe anafahamu,lakini kwa hali hii hapanaa
Mm nimekaa nachingwea, imenishangaza sana, ila Dr. Motto wa CDM anachukua jimbo mapema sana
 
Mm nimekaa nachingwea, imenishangaza sana, ila Dr. Motto wa CDM anachukua jimbo mapema sana
Nimeshangaa sana wana nachingwea kwa muamko huu ilibidi nipige simu kuuliza mbona hivi ?

Kuna wadau kanambia bwana mmoto anaweza kuchukua jimbo.

Na jambo baya zaidi yule mbunge wa CCM aliyepita ndugu masala alishinda kura za maoni lakini wakaja kumpitisha mtu ambae aliangika vibaya.

Sasa hatari zaidi huyo alopitishwa wana ccm wengi hawamtaki na sio mkazi wa pale kama masala anavyofahamika.

Jambo hilo limewafanya wanaccm na wapinzani wote waone kuwa bora kumpa mtu wa ypinzani tu kuliko kumpa jimbo mtu hawamjui
 
Dah maneno mazito haya yenye ukweli mchungu kwa wana-mtaa wa Lumumba kuwa wananchi wameamua sasa basi 2020 !

Babu yangu amenisimulia kuwa hivi hivi michango midogo midogo ya wananchi ndani ya "kapu la ukili " lilozungushwa kila baada ya mikutano ndiyo ilifanikisha Nyerere na timu yake kusonga mbele na kampeni na hatimaye Tanganyika kupata uhuru toka kwa mkoloni.
nakuambia siyo kazi rahisi wananchi wachangie wanasiasa ,hebu CCM wajaribu kwenye mikutano yao kama hawajachanga wale viongozi wakubwa tu wanaomwogopa magu
 
Back
Top Bottom