SIERA
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,789
- 3,413
Salama wakuu!
Ipo hivi najua kila mtu ashasikiliza ile album yake sasa mle naona kama kuna nyimbo nyingi nyingi kachukua beat mfano wimbo wa "body" harmonize ft burna boy, kachukua beat na neno "Show me the way" wa kwake Papa wemba, tuje wimbo wa Hainistui kachukua beat ya Mr nice na huyo hawakukubaliana chochote.
Bado subiri tena bado kuna ule wimbo wa Q chilla "Mabu" bado tena maneno yamerudiwa mule,. Sijamaliza kwanza kuna hii mpya ya Rosa lee kachukua beat tena, mpaka nyimbo ikafutwa kule YouTube,. Bado bado zipo ila tuishie hapo.
Ndo maana nikasema hiyo tabia inawezekana katoka nayo huko alikotoka kama alikuwa hamuoni boss wake akifanya hivyo maana mtoto lazima aige kwa baba, maana anaona jinsi anafanya na mbinu zote anajua[emoji41]
Yeye sio wakwanza wala wa mwisho... ukisikiliza nyimbo ya Diamond baba lao ni copy and paste ya nyimbo ya Naira malley wa Nigeria nahisi alimlipa maana ka copy Kila kitu mpaka video