POTOSHI Hii Taarifa ya GSM kujiuzulu ni ya mwaka 2025?

POTOSHI Hii Taarifa ya GSM kujiuzulu ni ya mwaka 2025?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Hii Taarifa ya GSM kujiuzulu ni ya mwaka huu?

GSM Aug 19.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Agosti 17, 2025 ilisambaa taarifa kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na Instagram ikieleza kuwa GSM

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa leo August 2025 limepokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC kutoka GSM "Tunaifanyia kazi barua hiyo na tutatoa taarifa kwa Wadau wa mpira wa miguu kuhusu suala hilo"​

#MillardAyoUPDATES Wana yanga wenzangu mdhamin kasepa tuanze kujitegemea Sijui tutaweza”​


Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya mwaka huu (2025).

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Taarifa hiyo ni Potoshi kwani si ya Agosti 2025 kama inavyoelezwa na badala yake imekuwepo mtandaoni kuanzia Februari 7, 2022.

Taarifa pamoja na grafiki hiyo ilichapishwa na Millard Ayo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii ikiwemo X ambapo Februari 7, 2022 alichapisha taarifa inayofanana na hiyo isipokuwa tarehe tu ambapo ya kwake katika upande wa tarehe ilisomeka “Februari 7, 2022”

"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa leo Feb 07, 2022 limepokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC kutoka GSM "Tunaifanyia kazi barua hiyo na tutatoa taarifa kwa Wadau wa mpira wa miguu kuhusu suala hilo"
Back
Top Bottom