Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Hii tabia imekuwa sugu; mtu anaamua tu aje Dar kukusalimia na afikie kwako

Akili yako na huyo jamaa yako zimefanana tu afu nyie mliopo Dar hamjui sikuhz mnadharaulika tu kama walivo wa Njombe huko au Katavi tu !? Mnajkuta wa juuu kumbe hovyo tu, kwa bandiko lako bora ungesema tu hauna ya kumlisha mtu usisema ety ghafla.
 
Sipendi kwenda kwa ndugu hata mtu akinialika niende kwake lazima nimtafutie sababu za kutokuja naona uvivu sana kwenda kwenye nyumba za watu.

Likewise mwenyewe sipendi kutembelewa na ndugu hata marafiki. Kila mtu aishi kwake.


Wewe ni mchoyo?

Unaogopa nini?

Unaficha nini?


Una mahusiano na jinsia tofauti na yako?
 
Mimi mtu hata akitoa taarifa kama anakuja kwangu simpokei. Utanipigia simu mpaka uchoke naicha tu inaita najua huyu atakuja ni mikosi na nuksi ndani kwangu.

Jifunze kujisimamia mwenyewe watu wako bize sana


Ni vizuri kuheshimu mipaka ya wenzetu, inatuepusha na mengi.



Lakini wewe kuna trauma imelala ndani yako, itibie.
 
Hii tabia imekuwa sugu. Yaani mtu anakaa tu na halmashauri ya kichwa chake anaamua kuwa nimpigie jamaa yangu yupo Dar nikafikie kwake.

Mi nipo zangu home jana inaingia simu ya Abouu. Ananiuliza maisha vipi namwambia safi tunalisongesha. Maneno maneno mengi mwisho anasema nipo Dar nataka nije kwako nielekeze. Nikamuuliza wakati unapanga kuja ulinishirikisha? Unaamua tu kuja kwangu hata hujanitaarifu.

Jamaa ame mind kawaambia watu nimemkataa. Ninyi wa Mikoani mnadhani huku ni kama kwenu huko ambako hamna ratiba maalum. Mnajiamulia tu.

Mwaka juzi nlimwacha mtu stand kwa upuuzi kama huo. Kakaa zake Mbwinde mwisho kaamua kuja town a anipigia simu kuwa yupo Dar anataka aje home. Nlimwambia tu kuwa sipo home na familia tumesafiri.

Akaanza kuomba basi nimpatie pesa ya sehemu ya kulala anisubiri. Nilimwambia mwezi mzima sitokuwa home. Akataka nimtumie nauli. Nlizima na simu kabisa. Huu ni wendawazimu.

Halafu tukiwaakaribisha mnaenda kutusema kijijini kuwa huku tunaishi maisha mazuri sana hatuwajali watu wa vijijini. Mnaenda kutuponda sana kijijini kuwa tunatumia pesa vibaya.




Mimi walienda kusema nafuja sana pesa badala ya kuwasomesha watoto wao. Mtu kazaa watoto 13 anataka nimsomeshee... Mimi nina 3 tu. Bado wanaenda kusema nakuaje na watoto wachache ... Mwanaume gani. Mke amenikalia kichwani anarudi jioni kama mwanaume. Wanataka wife awafulie nguo zao. Na wanakuwa wakali akirudi awapatie chakula n.k sina hamu na ndugu kabisa.

Mmoja tumekaa naye mwaka mmoja amekuja nimsomeshe diploma. Akirudi toka chuo anaangalia TV mpaka saa 4 akipewa kazi basi za home siku yupo asaidie... Anasema anateswa sana hawezi soma. Nikasubiri likizo. Akaenda kwao kusalimia. Nikamwambia atafute chuo aendelee kusoma huko, nitamlipia ada.

Alilia sana anataka arudi Dar. Nilimwambia huku wifi yako atakutesa hutapata muda wa kusoma. Akabembeleza sana nilimkatalia coz alishanipakaza sana kijijini na kumchafua sana wife. Na mtu mwenyewe ni ndugu wa mbali kabisa..

HAWA WAGENI WENGINE NDO HUNAJISI WATOTO NA UNDUGU UNAISHIA HAPO HAPO. MNAHARIBIANA FUTURE. KILA MTU AKAE KWAKE. DUNIA YA SASA IMANI IMEKWISHA. TUSAIDIANE KATIKA SHIDA LAKINI SI KUVAMIANA TU NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA UKARIMU. NDUGU WENYEWE IMANI IMEWATOKA. ANGALIA WANAOBAKWA, NAJISIWA AU LAWITIWA. MHUSIKA UTAKUTA BABA, BAMDOGO, MJOMBA, COUSIN NA JIRANI KWA MBALI KIDOGO.
Una hoja usikilizwe
 
Mimi nina wageni mwezi wa tatu unaingia najiuliza hawa washaweka kambi au laa
 
Back
Top Bottom