Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Watanzania tabia zetu nyingi zinafana, inapotokea ndugu, jamaa, mzazi au rafiki anaumwa na pengine kulazwa wengi wetu hawajigusi, sana sana mtu atajitahidi atapiga simu mara mbili kuulizia hali ya mgonjwa basi baada ya hapo anakata mawasiliano.
Sasa inapotokea mgonjwa yule kafariki wengine hupanda hadi ndege kwenda kwenye maziko, na wengine wanajaza magari yao wese hadi huko msibani ilhali muda ule msaada wako wa pesa ulihitajika kwa ajili ya kuokoa maisha ya mgonjwa ulikuwa unasema upo busy.
Mwaka jana kuna msiba ulitokea mtaa wa jirani, huyo baba aliumwa sana lakini watoto wake wengi hata hawakusafiri kwenda kumuona hata pesa wengine walikuwa hawatumi. Basi bwana mwisho wa siku yule mzee akafariki. Watoto wote na ndugu wakasafiri kwenda msibani wakaandaa mabufee ya pilau ndizi na wali, baada ya Padre kumaliza kusoma ibada ya mazishi alikaribishwa chakula lakini akasema pale pale msibani yeye hatokula kwa sababu hiyo familia imepata pesa ya kuaandaa chakula kingi na kizuri lakini lakini kwenye kumuuguza baba yao pesa hawakutuma hadi mzee akapata umauti kwa kukosa huduma nzuri ya afya.
Jamani wandugu tubadilike maisha hayapo hivyo. Huu si uungwana.