Swali: Je, sayansi inaweza zimwa na uchawi? nimeuliza swali ili kutokana na maelezo ya wadau hapo juu, maana kilichotengeneza gari ni sayansi, na kinachofanya gari lisiweze kuendelea na safari ni nguvu za giza,(UCHAWI). Huko Nachingwea kuna sehemu kunaitwa farm 17, (Shamba la kumi na saba) huko kulikua na mzee, akiomba lifti kwenye Baiskeli yako ukimnyima, ukiondoka zako, utakuawa peke yako, ila kitendo cha kufika Nachingwea mjini, kama ulielekea huko, utasikia mtu anatoa shukrani kwa kumbeba kwenye baiskeli yako. ukigeuka kuangalia anaetoa shukrani, kumbe ni yule mzee ulimkatalia kumbeba, kule farm17.