Hii Teknolojia ilikuwepo Enzi zile za Umwinyi Mikoa ya Pwani. Nahisi Wazungu waliiba kwetu

Hii Teknolojia ilikuwepo Enzi zile za Umwinyi Mikoa ya Pwani. Nahisi Wazungu waliiba kwetu

Dah....Mamwinyi walikuwa wengi hatari kila sehemu na vimbwanga vyake na watabe wake kwenye sector hiyo
Achana na Mamwinyi... kwa mfano mimi Babu yangu alikuwa full Mwarabu kasoro rangi tu!!! Mamangu anasema hadi Baba ake amefariki hakuwahi kumsikia akiongea kilugha cha kwao! Mwinyi aongee kilugha... thubutu!!!! Tusi lake kubwa lilikuwa "shet'waani mkubwa wewe!" Halafu hiyo "shet'waani" ina swaga zake za kuitamka na sio unaitamka kama mtu wa "maporini!"
 
Swali: Je, sayansi inaweza zimwa na uchawi? nimeuliza swali ili kutokana na maelezo ya wadau hapo juu, maana kilichotengeneza gari ni sayansi, na kinachofanya gari lisiweze kuendelea na safari ni nguvu za giza,(UCHAWI). Huko Nachingwea kuna sehemu kunaitwa farm 17, (Shamba la kumi na saba) huko kulikua na mzee, akiomba lifti kwenye Baiskeli yako ukimnyima, ukiondoka zako, utakuawa peke yako, ila kitendo cha kufika Nachingwea mjini, kama ulielekea huko, utasikia mtu anatoa shukrani kwa kumbeba kwenye baiskeli yako. ukigeuka kuangalia anaetoa shukrani, kumbe ni yule mzee ulimkatalia kumbeba, kule farm17.
 
sio uchochezi jamani, mbona mara nyingi hao wazee ni waislam tuu?
 
Umenikumbusha simulizi kutoka kwa mkuu fulani wa Wilaya (Mungu amuweke mahali pema)

Baada ya kupata huamisho kutoka Mkoa fulani (jina kapuni)
na kupelekwa katika Wilaya nyingine Mkoani Kigoma.

Alifika, na kuanza kutekeleza majukumu yake mapya aliyo pangiwa.

Baada ya siku kadhaa kupita, alitembelewa na Mgeni fulani mtu wa MAKAMO.

Mgeni/Mzee huyo alimsabahi (DC) na kujitambulisha, alipokaribishwa KITI, Kabla ajaketi, alivua KOTI lake na KOFIA (Balaghashea) na kuvitupia UKUTANI.

Baada ya maongezi marefu, akimueleza historia ya Mkoa, Wilaya anayo iongoza, tabia za Wakaazi na mengine mengi.

Mzee yule alimuaga Mgeni (DC) na kwenda zake huku akimuahidi kurudi kumtembelea siku nyingine.

Kilicho fuata sasa, yule Mkuu wa Wilaya (Marehemu) alianza malalamiko na visingizio vingi akimuomba Mkuu wa Kaya (kipindi hicho) amfanyie HURUMA kumuamisha katika Majukumu/ Wilaya nyingine.

Kweli, nafikiri uwezekano wa kuwapata wazee, kukaa nao chini, kuzungumzia uwezo na uboreshaji wa Taaluma hiyo, ni jambo la msingi.

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
867872d133a06887c02708eaabf53b62.jpg


Baada ya kutupa/kurusha Koti na Kofia yake, vilinasa pasipo kuwa na kitu cha kushikilia, mfano Msumari ama Henga.

(Sentensi hii ilikosekana katika mchango/post yangu)

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
Hahahahaaa hawa watu noma aise sasa ukitaka kujua hawafai litisha gari lako uwanjan kwake akuambie alaf umjibu shit ndio utajua gari inanasa hata katika lami mpaka uombe msamah akuonee huruma

Sent from my RIDGE 4G using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka nilisimuliwa kisa fulani na jamaa yangu mmoja ambae alikuwa anaenda Tanga kununua machungwa.....sehemu moja inaitwa Muheza huko ndani ndani huko.....

Walifika kwa mzee wakapatana bei kabisa na vijana wake wakaanza kuchuma na fuso letu.....wakati wote yule mzee alikuwa ndani tu maana ilikuwa ni asubuhi na palikuwa na ukungu ukungu hivi.........na kaubaridi baridi....

Sasa vijana baada ya kuona mzee hashughuliki nao wao wakajiongeza machungwa mengi sana tofauti na idadi waliyokubaliana na yule mzee kulingana na pesa yao.....

Walimaliza wakafunga vizuri wakijiandaa kuondoka....wakamuaga na babu ambaye mpaka muda huo alikuwa bado yupo ndani.......wale vijana walipo maliza kufunga wakaenda kuwasha gari lakini gari halikuwaka....walihangaika sana lakini mambo yakawa ni yale yale tu.......

Mpaka yule mzee alipoamka na kwenda kuwauliza kuwa kwani mmepakia machungwa mangapi....vijana wakajibu ni yale yale mzee.....

Mzee akawaambia hembu mwageni alafu muhesabu tena...moja baada ya jingine....

Vijana wakafanya hivyo kwa shingo upande....wakati wanahesabu yale machungwa ilipotimia ile idadi tu mzee akawaambia nendeni mkawashe gari....cha ajabu ile gari iliwaka vizuri kabisa....lakini wakirushia chungwa hata moja haliwaki au hata kama lilikuwa lina waka linazima hapo hapo......

Tanga kuna mambo....
 
sio uchochezi jamani, mbona mara nyingi hao wazee ni waislam tuu?

Mkuu swali lako ni la msingi lakini hapa si mahala pake....unaweza ukaamsha mambo ya ubishani wa kidini na tukatoka nje ya dhumuni la mada....
 
Bora hata kwenu mlikuwa mnakuta vitu hivyo na mkigundua mnasubiri wahusika,sisi kwetu mpaka leo hii mtu ukitaka kusafiri mda wowote ukifika stendi instantly gari nayo ndo inafika mda huo mnaondoka,yani hiyo mechanism ya kucheleweshwa huko mlikokuwa mkitoka muhusika anajua mwenyew, yani hata aseme aondoke saa 10 za asubuh bado nanyie ndo mtakuwa mnafika eneo lile
 
Mikoa iliyokuwa na watu wa tabia ukiifatilia sana mpk sasa maendeleo yao ni ya kusuasua
 
Kama ndiyo hivyo mbona walishindwa kuwachachafya wakoloni walio watesa na kuwaonea? Kwa nini hawaku-waadabisha wazungu kwa kutumia elimu yao?
Swali zuri, waarabu na wajerumani ndo waliowafunza waafrica ulozi
 
umenkumbsha wanyak mwaka iyo, kma kuna sehem kuna mzee/wazee wamekaa we ukapta na gar au baiskel bila kuwasalimia, kuna mawil, kupata kaajal kadogo mbele kdogo au gari kuzma we waibaisker kuna pacha au break kukatka ukaanguke. Hi ki2 ilweka heshma sana kwa vjana. Endapo ungesmama na kuwasalimia safar yako itaendelea vzur kabsa
Hiyo si heshima bali shuruti.
 
Acheni hizo stori za vijiwe vya kahawa. Ukimuuliza mleta stori wewe uliona utasikia kanisimulia mzee flani n.k.
Ugunduzi wa remote umewezeshwa na nadharia safi kisha ukahitimishwa na mbinu za utengenezaji kwa vitendo.
Kikubwa zaidi umetumia scientific methods/procedures.

Unajua scientific methods sifa yake?
ni kuwa yeyeyote akifuata hizo procedure/taratibu zilizo andikwa basi lazima atafikia matokeo yaleyale hata kama akirudia mara elfu moja au wakijaribu watu milioni mia moja.

Hizi njia zenu za mamwinyi hazina nadharia wala vitendo na sio kila mtu atakaejaribu kufuata hatua hizo atafikia matokeo au jibu hilohilo. It's a fvcking hoax!! Damn fvcking myth.
 
Back
Top Bottom