- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Baada ya Rais wa zamani na mgombea urais kwa tiketi ya Republic bwana Trump kukoswa koswa na risasi kuna video nyingine nimeiona akipigwa kofi akihutubia.
Nimepita kwenye baadhi ya mitandao sijaona hilo tukio. Hili tukio ni la kweli na kama ni la kweli, lilitokea lini?
Video husika
Picha ya video
Nimepita kwenye baadhi ya mitandao sijaona hilo tukio. Hili tukio ni la kweli na kama ni la kweli, lilitokea lini?
Video husika
Picha ya video
- Tunachokijua
- Mgombea urais kupitia chama cha Republican katika uchaguzi ujao nchini Marekani na Rais wa zamani Donald Trump alishambuliwa kwa risasi kadhaa akiwa katika mkutano mjini Butler Pennsylvania Julai 14, 2024
Walinzi wake walimzunguka na kumuinua baada ya kuanguka chini huku akionekana kuvuja damu upande wa sikio la kulia baada ya milio ya risasi kadhaa kusikika mkutanoni.
Kijana wa miaka 20 aliyedaiwa kuhusika shambulio la Trump aliuawa baada wakati wa shambulio hilo.
Siku chache baada ya shambulio hili, video inayomuonesha Trump akipigwa kofi wakati akihutubia ilianza kusambaa mtandaoni, na baadhi ya Akaunti zilizochapisha video hizi zimehifadhiwa hapa, hapa na hapa.
Video hii ni halisi?
Ufuatiliaji wa JamiCheck umebaini video hii ni halisi, lakini imehaririwa.
Utafutaji wa kimtandao wa kutumia Google Image Search umeonesha video hii iliwahi kuchapishwa kwenye Mtandao wa YouTube na chaneli ya Shirika la Utangazaji la CBS News, Machi 16, 2026 ikiwa na kichwa cha habari "Watch: Secret Service run to Trump as protester rushes stage"
Kwa mujibu wa maelezo ya video halisi, tukio hili lilitokea baada ya mwandamanaji kwenye mkutano wake huko Vandalia, Ohio, kujaribu kupanda jukwaani. Baada ya kudhibitiwa kwa mwandamanaji huyo, Trump alisema alikuwa "tayari" kumkabili lakini alikubali kwamba ni bora usalama washughulikie tukio hilo.
Kwenye video hii, Trump haonekani akipigwa kofi la mgongoni tofauti na video inayosambazwa mtandaoni.
Utafutaji mwingine wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu umebaini tukio hili lilifafanuliwa pia kwenye gazeti la NBS News Machi 12, 2016 ambapo pamoja na mambo mengine, gazeti hili lilimnukuu Mkuu wa Polisi akisema Mtuhumiwa aliyetambuliwa kama Thomas Dimassimo, mwenye umri wa miaka 32, alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuvuruga amani na kusababisha hofu.