Hii vita ya ubingwa wa Yanga na Simba, hivi TAKUKURU hamsikii kelele za waamuzi kupozwa ligi kuu?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Bongo buana mambo ni mengiiiii lakini muda mchache, ndiyo maana wanasema ukiishi Bongo ukifa kwa stress basi wewe jua umejitakia.

Ligi yetu inaendelea, sasa hivi kuna kurushiana maneno mitandaoni na kwenye vyombo vya Habari hasa Yanga, Simba na kidogo Azam FC wanasikika kwa mbali.

Mtaani tunajua kuwa hizo kelele zote unazozisikia ni kuwa kuwa wanazidiana nguvu kwenye kuwapa mpunga waamuzi ili wawabebe,,,,

Inajulikana klab hizo kubwa kwenye suala la kutoa mpunga kwa wapuliza filimbi ni jambo la kawaida.

Mi nadhani imefika hatua waamuzi nao waanze kutoaau kufichua miamala wanayoumiwa na watu hao wa soka, inachekeshaaa, kama haiwezekani vile lakini kama wakiamua kutoa angalau robo tu ya miamala inayohama kutoka upnde mmoja kwenda mwingine nchi hii itageuka.

Hivi najiuliza TAKUKURU mko wapi ndugu zangu, hizi mambo hamzisikii au labda mnaona haya mambo ya mipira hayawahusu.

Inabidi ifike hatua sasa na nyie tukawasemee kwa mama Samia, maana maneno mtaani ni mengi na hata hao wanaoendesha soka wanajisahau kuna muda wanabwatuka kabisa kuhusu uwepo wa mazingira ya mkono wa nyuma.

Serikali amkeni amkeni kwenye soka huku kumeozaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…