Hii ya Ajib inanihuzunisha.

Hii ya Ajib inanihuzunisha.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Nimesikia leo kuwa mchezaji Ibrahim Ajib wa klabu ya Yanga kaomba asicheze mechi leo dhidi ya KMC kwa kuwa anaumwa.
Nimekuwa natafakari sana suala hili kwani mie hupendelea sana kumuona akicheza uwanjani. Ni kawaida mchezaji kutaka acheze mechi kwani ndo shughuri yake na kutocheza mechi ni daktari na koca ndio huamua mchezaji asicheze mechi kwa sababu za ugonjwa au ufundi.
Hii ya Ajib, kali!!!!!!!!
 
Huyu dogo ana mpira lakini hajitambui
Sawia mkuu ila nashawishika kuamini pana mtu/watu wanaompotosha kwa kuwasikiliza nje na maelekezo ya kocha wa timu.
 
Mwacheni apumzike anabeba Mzigo wa timu nzima! Bila yeye ndala fc ni mdebwedo, kama umeangalia mechi ya leo utakuwa umeliona Hilo!
 
inawezekana mganga wake kamwambia halafu yanga timu ya ajabu kawaida daktari wa timu ndiye anatoa ripoti kwa kocha wachezaji gani wazima au wagonjwa ila la ajibu linaweza kuwa ajabu la nane duniani yeye ndio anamwambia kocha anaumwa ina maana yanga hawana daktari wa timu
 
ndio anaumwa kwa hiyo nini kwani au yeye ni robot eee nauliza mikia fc ,wale kmc walikamia sana mechi ya jana lakini wakaachia tu.kaseja amekoswa nyingi sana sana
 
inawezekana mganga wake kamwambia halafu yanga timu ya ajabu kawaida daktari wa timu ndiye anatoa ripoti kwa kocha wachezaji gani wazima au wagonjwa ila la ajibu linaweza kuwa ajabu la nane duniani yeye ndio anamwambia kocha anaumwa ina maana yanga hawana daktari wa timu
Mkuu, inawezekana baada ya waandishi kumpamba akaona (shauriwa) apime kina cha maji kwnye mechi hii.
Mungu si Athumani kaumbuka kwa Yanga kushinda ila ingetoka sare au kufungwa pasingelalika Yanga na timu ya Taifa.
 
Kingereza????Halafu unamkosoa mtu.Hicho nacho kiswahili???
 
Back
Top Bottom