Hii ya makato ya VAT inakuaje?

Hii ya makato ya VAT inakuaje?

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
34,962
Reaction score
70,576
Hello.

Jamani nimeenda sehemu fulani kupata chakula na vinywaji, lakini bill ilivyokuja nikashangaa kila kitu kimekuja kwa receipt yake na kila kinywaji kina VAT yake!

Mfano: Soda 4 zimekuja receipt mbili za soda mbili mbili. Chakula kimejua na receipt yake na VAT yake!

Swali je ni sawa? Kwanini kama bill ni 1000/= kwanini isingekata hiyo VAT yao kwenye hiyo 1000/=? Means nimeletewa receipt 6 kila receipt ina VAT yake!

Naomba wataalamu wanieleweshe hapa kama ni sawa au kuna upigaji umetokea!
Hasira za Sumaye nizimalizie hapa hapa leo hotelini!
 
Elimu yako tafadhali? VAT inakatwa kwa asilimia. Ni 18% ya gharama uliyotumia. Hivyo basi haijalishi una risiti ngapi, ziwe mbili, moja au tatu..mwisho wa siku kiasi utakacholipa ni kilekile
 
Std7!hapana hujaelewa aisee mkuu...haiko sawa!na ilibidi tuulize..wakarekebisha
 
Basi pengine hujajieleza vizuri. Maana hoja yako ya msingi iko kwenye idadi ya risiti. Hebu fafanua ili tuweze kuelewa nini hasa kilitokea.
 
Bili imekuja imetenganishwa..na kila bill imekatwa vat..hawakuicompile..kiliniuma..nikajikaza kuuliza😅!wakaona wenyewe wamekosea!
 
Hizo bill ziliandikwa na mkono au mashine. Kama ni mashine basi Jumla ya VAT itakuwa ni ile ile bila kujali idadi ya risiti.

Chukua mfano huu nimekula chakula cha 3000 na juice ya 2000, jumla 5000. Nikiandikiwa risiti moja itakuwa 5000 + VAT = 5000+900 = 5900. Nitalipa 5900.

Nikiandikiwa risiti mbili:
1. Chakula 3000+540 = 3,540.
2. Kinywaji 2000+360 = 2,360

Ukijumlisha risiti zote mbili 5,900. Mzee baba unakwama wapi?
 
😅😅!...wenyewe waliona kun kosa..au la hujaelewa!asante pia
 
Wewe umeomba wataalamu tukueleweshe. Ni vyema ukajieleza vizuri. Kosa lilikuwa wapi? Na ulitakiwa ulipe shs ngapi kabla ya kurekebushwa? Na baada ya kurekebishwa ukalipa shs ngapi?
 
Pointi ilikua zilikuja risiti 6! Kwann wasijumulishe tu zote!ktk calculation zao za VAT nikawa nimekatwa twice!
 
Elimu yako tafadhali? VAT inakatwa kwa asilimia. Ni 18% ya gharama uliyotumia. Hivyo basi haijalishi una risiti ngapi, ziwe mbili, moja au tatu..mwisho wa siku kiasi utakacholipa ni kilekile
Ukurupukaji hajui kuwa ukijumlisha zote ni sawa na kukata kwa ujumla. Ujuaji mwingi nakuelezaga manengelo
 
1. Ufafanuzi wa kwa nini alipata risiti zaidi ya moja unatokana na usajili. Hii ina maana ya kwamba wakati unasajili VAT huwa unatakiwa kutoa list ya huduma/bidhaa ambazo utakuwa unahudumu/unauza. Hivyo utaona walimpa risit kutokana na namba za usajili wa bidhaa tajwa. Mara nyingi huwa tunapewa risit ambayo inajumuisha kila kitu kwa muuzaji kuandika mfano bidhaa/huduma ie kama angeandika zote ingekuwa soft drinks lkn kuna wateja watata hutaka kila bidhaa apate risit yake japo pia waweza kuandika risit moja yenye kila bidhaa/huduma inategemea na mhudumu anaekutolea risit kama anajua au laa kutoa risit yenye items zote kwa kuainisha moja moja ktk risit moja tu

2. Mkuu iMind concept yako ya VAT ni sahihi pia
 
Hello.

Jamani nimeenda sehemu fulani kupata chakula na vinywaji, lakini bill ilivyokuja nikashangaa kila kitu kimekuja kwa receipt yake na kila kinywaji kina VAT yake!

Mfano: Soda 4 zimekuja receipt mbili za soda mbili mbili. Chakula kimejua na receipt yake na VAT yake!

Swali je ni sawa? Kwanini kama bill ni 1000/= kwanini isingekata hiyo VAT yao kwenye hiyo 1000/=? Means nimeletewa receipt 6 kila receipt ina VAT yake!

Naomba wataalamu wanieleweshe hapa kama ni sawa au kuna upigaji umetokea!
Hasira za Sumaye nizimalizie hapa hapa leo hotelini!
Inategemea mtu aliyekuandikia risiti hawezi kuzitofautisha kwa kila items katika risiti moja ila akaamua kutoa kila item na risiti yake ,mwisho wa siku ukijumulisha total amount inakuja sawa na uliyotoa mkuu.
 
No haina upigaji coz jumla ya hizo VAT ni sawa na ambayo wangeicompile ,ila huenda uliagiza soda 2 kwanza so wakawa wameshatoa receipt ya soda ,then Chakula baadaye pia wakaitoa, so wamekuletea receipt 2 za wakati tofauti tofauti,

kama ni Kwa wakati mmoja inabidi wajifunze kufanya paper saving,maana hivo vikaratasi vinauzwa(fiscal paper rolls) hakukua na ulazima Wa kutoa receipts zote hizoo
 
Yaani ilibidi niulize kwanza..wakaja na fig zingine kuhusu hyo18%yao
 
😅😅!...wenyewe waliona kun kosa..au la hujaelewa!asante pia
Natamani kujua walikoseaje...manake hata watoe risiti idadi watakayo, kiwango cha VAT kitabaki kuwa kile kile. Labda mtoa risiti aliona amekosea kutoa risiti tatu za soda hivyo akarekebisha kwa kutoa moja...
 
Zile vat walipiga dabo dabo😇!
 
Kuna makosa yamefanyika hapo... Umeibiwa...

Kama soda ni 500/=, wewe unapaswa kulipa 500/= hiyo hiyo, VAT tayari ipo kwenye hiyo 500/=... siyo akuambie 590/=

Itakua hajui kutumia EFD machine huyo...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom