Hii ya Mtoto kufa baadae kuonekana hai tuiitaje

Mpanda nyangobe

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
762
Reaction score
1,688
Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji cha Ngemo kata Ngemo Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amezua taharuki kwa kuonekana hai tena baada ya kufariki miaka
minne iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita, Kamishana msaidiizi Henry Mwaibambe
amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana
tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktober 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua tarehe 12 Desemba mwaka huu.

Katika maelezo yake ACP Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika
kwa jina a la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku Wala vipande vya kanga
ambavyo mama amedai walimzikia mwane miaka minne iliyopita.

Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo kwa sasa haongei
baada ya kuonekana hai huku ulimi wake ukiwa umekatwa.

My take: Kama madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya mkoani Geita walithibitisha kifo cha huyo dogo ..lakini amepatikana hai basi naamini waafrika tupo mbali sana kiteknologia Ila tuko underrated na wazungu
 
Kwani daktari bingwa na mbobezi wa huko anasema je?

IMG_20211212_224003_053.jpg
 
Ni porojo tu, hakuna mtu anayekufa halafu akafufuka.
 
Wachawi walimficha. Hayo mambo mbona yapo mengi hasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Kuna mzee aliwahi kuniambia kuna siku aliona kabisa watu wakizika shina la mgomba na majani yake huku wakijua wanazika mwili wa mtu. Kumne mtu mwenyewe, wachawi wanaye. Na wanamkata ulimi kama walivyosema kwa huyo mtoto.
 
Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji cha Ngemo kata Ngemo Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amezua taharuki kwa kuonekana hai tena baada ya kufariki miaka
minne iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita, Kamishana msaidiizi Henry Mwaibambe
amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana
tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktober 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua tarehe 12 Desemba mwaka huu.

Katika maelezo yake ACP Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika
kwa jina a la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku Wala vipande vya kanga
ambavyo mama amedai walimzikia mwane miaka minne iliyopita.

Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo kwa sasa haongei
baada ya kuonekana hai huku ulimi wake ukiwa umekatwa.

My take: Kama madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya mkoani Geita walithibitisha kifo cha huyo dogo ..lakini amepatikana hai basi naamini waafrika tupo mbali sana kiteknologia Ila tuko underrated na wazungu
Tunaomba death certicate yake na picha msiba wake
 
Hayo mambo ya kuchukuana msukule,kwa upande wa mikoa ya kanda ya ziwa yapo sana. Nafikiri sababu kubwa ni madini. Wasukuma wako njema kwa mambo hayo
 
Tatizo lililopo kuna baadhi ya watu hawaamin uchawi ila uchawi upo kabisa,hivyo kwa hili kuna watakaosema ni uongo na wapp wataosema ni kweli hiv mtu unakataa vip wakati unaelezwa alizikwa miaka 4 iliyopita tena Geita ila kapatikana Kahama mtu anabisha,uchaw upo tuu
 
Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji cha Ngemo kata Ngemo Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amezua taharuki kwa kuonekana hai tena baada ya kufariki miaka
minne iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita, Kamishana msaidiizi Henry Mwaibambe
amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana
tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktober 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua tarehe 12 Desemba mwaka huu.

Katika maelezo yake ACP Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika
kwa jina a la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku Wala vipande vya kanga
ambavyo mama amedai walimzikia mwane miaka minne iliyopita.

Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo kwa sasa haongei
baada ya kuonekana hai huku ulimi wake ukiwa umekatwa.

My take: Kama madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya mkoani Geita walithibitisha kifo cha huyo dogo ..lakini amepatikana hai basi naamini waafrika tupo mbali sana kiteknologia Ila tuko underrated na wazungu
Je, aliugua kabla ya ''kufariki''. Na kama aliugua, alitibiwa wapi? Rekodi zake zipo? Kuna cheti cha kifo? Kuna picha za mazishi? Mazishi yalihudhuriwa na watu gani na wanaweza kutoa ushahidi pasipo shaka? Possibly hii ni janja ya watu fulani kutengeneza mazingira.....
 
Mojawapo ya athari za kupewa taarifa ni kulazimika kuipokea taarifa kama ilivyo. Ila ukishuka chini mwenyewe utakutana na yafuatayo:
1. Taarifa ya kweli na ndo ukweli
2. Taarifa ya kweli lakin maelezo si kweli.
3. taarifa si ya kweli na maelezo ni ya kweli.
4. Taarifa si kweli na maelezo si kweli.
Katika dunia hii wengi tuna taarifa ni kweli, maelezo si kweli.
mf. Juzi taarifa ya mtu nyumba yake kuungua moto musoma ni kweli lakin maelezo si sahihi. Ni suala la mtu kukutangulia akili.
 
Mie kwa vile niliwah rogwa na nikaenda kwa Dr hospital ya misheni akanishauri niende kwa mganga wa kienyeji nikaenda na nikapona naamini uchawi upo hata madaktari wanayajua hayaa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Ni porojo tu, hakuna mtu anayekufa halafu akafufuka.
Muone huyu mzungu naye [emoji1787][emoji1787]

Iko hivi, jamii nyingo za Kiafrika zina imani zake ikiwemo uganga na uchawi. Kwa kanda ya ziwa, mambo kama haya yaliyotokea huko Mbogwe si kitu cha kustaajabisha huko kwani mambo haua huwa yapo.

Kinachofanyika na wachawi ambao wanakuwa wamekupenda/ kukuhitaji kwenye kazi zao wanakuchukua japo kwa nguvu za giza, yaani unakuwa umekufa na unazikwa kama kawaida but katika ulimwengu wao unakuwa hai japo wanakuzezetesha/ unakuwa haujitambui wanakukata ULIMI na kuna madawa yao wanajua wanakupa ili usiwe na fahamu.

Niliwahi kusimuliwa na babu yangu kwamba, kitendo hiki hufanyika pale tu wanapokuwa wamekupenda uwafanyie kazi zao unakuwa LITUNGE/LITUNGA Kama sijakosea kwa lugha ya kisukuma hivyo wanakutumikisha na mabibi wengi wako vile, wanaingia gharama kukulisha na inasemekana kazi huwa ni pamoja na kulima.

Niliwahi kusikiliza "story" ya Zabron kupitia Radio Free Africa kipindi cha sintosahau aise ilikuwa hatari, yule bwana alichukuliwa ila alibahatika hakukatwa ulimi ndio maana alitambua kila kitu kinachofanyikaga huko. Kwakwei nilijifunza mengi sana juu ya teknolojia hiyo.

Kufupisha story, mambo haya yalikuwepo na bado yataendelea kuwepo, mara nyingi huwa inatokea misibani mnazika mbwa, punda na wakati mwingine vitu vya ajabu lakini mnakuwa hamfahamu Hadi utakapotumia dawa zao za utambuzi.

Vifo vingi sana hasa kanda hiyo huwa hawaini kama mtu huyo hajalogwa,, kuna mtu aliwahi kunisimulia pia kwamba waganga wa jadi muda mwingine huwa wana NEGOTIATE na wachawi kwasababu nguvu huwa zinavutana, kuna kipindi yule mganga alikuwa anasumbuliwa wanamwambia tunaomba utuachie huyu mtu tunamhitaji sana, mara zote unakuta ndugu zake wanamtoa kafara. Ni mambo mengi ya kuongofya but hali ndio hiyo.

Uchawi upo na ndio identify ya mwafirka, sijui kwanini Wachawi wazungu waliamua kuwaita WITCH DOCTORS wakati wao wakajiita MEDICAL DOCTORS.

Hope Kaka yangu Mshana ataongezea nyama.
 
Hiyo ndo sayansi pekee anayojivunia mwafrika, hadi kufikia maendeleo ya mtu mweupe labda ije dunia mpya.
 
Back
Top Bottom