Hii ya tezi dume Imenishtua kidogo

Hapa nathibitisha kauli ya Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump kuwa Waafrika wanawaza ngono tu. Yaani watu mko tayari kurisk kifo kwa sababu ya hofu ya kupungua nguvu za kiume!

Kaaz kwelikweli.


Vv
 
Kwahiyo mtu anaona bora afe na uanaume wake kuliko atibiwe!!! Aiseeee!!! Saaaaaasa mama naniliu inakuwaje!!

Atoto, madai ya Trump dhidi ya Waafrika yanathibitishwa ktk hilo. That's Trump's theory on Africans and sex.

Vv
 
Kwahiyo mtu anaona bora afe na uanaume wake kuliko atibiwe!!! Aiseeee!!! Saaaaaasa mama naniliu inakuwaje!!
Sijui huu ugonjwa unasababishwa na nini , na waheshimiwa wengi wameondoka nao wengine wapo na wamefanyiwa operation
 
Ukurupukaji wa kiwango cha lami.
Tofautisha ugonjwa wa tezi dune na kansa ya tezi dume.
Jk alikuwa na tatizo la tezi dume na si tatizo la kansa ya tezi dume.

Huyo mama kazungumzia tatizo la kansa ya tezi dume

Ulichoandika ni sahihi kabisa.

Ugonjwa wa Tezi dume (Benign Prostatic Hyperplasia - BPH) ni ugonjwa wa kawaida wa Tezi Dume na si ugonjwa wa saratani kama wengi humu wanavyotaka kuamini.

BPH (kuvimba kwa Tezi Dume) ni ugonjwa unaoshabulia wanaume wa makamo (zaidi ya miaka 50) ambao hauhatarishi maisha. Chanzo chake hakieleweki, lakini wataalamu wanaamini ni kwa sababu ya mabadiliko ya 'homone' mwilini kutokana na umri.

BPH inatibiwa kwa upasuaji. Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH huchukua muda fulani (inategemea umri na afya ya mgonjwa husika) kuweza kurudia hali yao ya urijali. Ila wengi wao pia huwafanya kuwa wagumba, japo wanakuwa rijali.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya BPH na saratani ya Tezi Dume japo dalili zinafanana. Kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume.

Inashauriwa, wanaume wote wenye umri zaidi ya umri wa kuanzia miaka 40, kufanya uchunguzi wa Tezi Dume zao, walau mara moja kila mwaka.

Mwenye kutaka kujua zaidi asome kuhusu BPH.
 
Dr.Kombe juzi alielezea kwa kina.Ila pamoja na hayo pombe,kuchanganya wanawake kunachangia sana!
 
Ila unapata retrograde ejaculation. No discussion on that
"Retrograde ejaculatulion" ni kilele (mshindo) kikavu (shahawa zisizo na mbegu).

Upasuaji wa BPH huondoa misuli maalumu ambayo hufunga kijitundu cha kutoa mbegu zisingie kwenye kibofu cha mkojo badala yake ziungane na shahawa kwenye njia ya mkojo wakati wa kilele (mshindo) kwenye tendo la ndoa.
 
Ukurupukaji wa kiwango cha lami.
Tofautisha ugonjwa wa tezi dune na kansa ya tezi dume.
Jk alikuwa na tatizo la tezi dume na si tatizo la kansa ya tezi dume.

Huyo mama kazungumzia tatizo la kansa ya tezi dume
HE!
 

Kuna upimaji mbadala ambao wanachukua damu na kupima kitu inaitwa PSA!! Lakini kwa usahihi na uhakika wa kupima hilo tatizo upimaji wa kuingiza vidole njia ya haja kubwa ndio unaoaminiwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…